loader
Picha

Wataka masharti magumu viwanda vya kuchakata nyama ya punda

SERIKALI imeombwa iweke masharti magumu kwa viwanda hivyo vinavyochakata nyama ya punda na ngozi zake ili kudhibiti wizi mkubwa wa wanyama hao unatokea kwa sasa. Hiyo inatokana na uchinjaji wa wanyama hao kuanza kusababisha wizi katika vijiji vya Migoli na Makatapola wilayani Iringa.

Vijiji hivyo hutegemea wanyama hao kwa ajili ya ubebaji wa mizigo ili kuendesha maisha yao. Kauli hiyo imetolewa na wafugaji katika sherehe ya Siku ya Kimataifa ya Punda iliyofanyika Mei 17.

Siku hiyo inaadhimishwa kutambua thamani kubwa aliyonayo mnayama huyo kwa binadamu katika kufanikisha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Walisema kuwa viwanda vya ngozi ya mnyama punda vilivyopo katika mikoa ya Dodoma na Shinyanga vinachochea wizi wanyama hao na kuathiri ustawi wa familia zinazotegemea kuwatumia kuendesha maisha.

“Kama hakutakuwa na sheria kali ya kumlinda mnyama huyu upo uwezekano akatoweka katika ardhi ya Tanzania na kumfanya kuwa mnyama adimu nchini,” alisema Mkazi wa Mtera, kata ya Migoli, Robert Geitani ambaye pia alishauri serikali itilie mkazo utekelezaji wa sheria ndogondogo za vijiji zinazokataza wanyama mbalimbali wa kufugwa wakiwemo punda kuzurura ili kuwalinda dhidi ya uhalifu huo na hata ajali za barabarani.

Alisema sheria hizo zikitiliwa mkazo zitapunguza ajali za punda zinatokea katika maeneo kama Iringa, Dodoma na Singida wanakofugwa kwa wingi. Mkazi mwingine wa Kijiji cha Mtera, Mario Katemba alisema mnyama huyo ni msaada mkubwa kwa wakulima na kusema kwa sasa anastahili kulindwa kutokana na spidi ya kuibiwa kwake kutoka kwa wanaowafuga.

Ofisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya Iringa, Isidory Karia, ambaye pia mratibu wa mradi wa kuboresha maisha kupitia ustawishaji punda ngazi ya wilaya unaofadhiliwa na Indades Formation Tanzania alisema shirika hilo limesaidia kuboresha maisha kupitia ustawishaji wa punda.

Alisema wananchi wanaotoka katika vijiji vya mradi vya Migoli na Makatapola wameelewa umuhimu wa punda pamoja na haki zake na akaiomba serikali kukomesha au kuzuia kwa muda biashara ya ngozi yake kwani inahatarisha uwepo wa mnyama huyo.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema tangu awe Waziri hajawahi ...

foto
Mwandishi: Frank Leonard, Iringa

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi