loader
Picha

Muhongo kugawa majembe 40 ya kukokotwa na ng’ombe

MBUNGE wa Musoma Vijijini mkoani Mara, Profesa Sospeter Muhongo (pichani), anatarajia kugawa majembe 40 ya kukokotwa na ng’ombe kwa vikundi mbalimbali vya wakulima jimboni mwake wakati wa Sikukuu ya Idd El-fi tri.

Akizungumza na gazeti hili, alisema vikundi hivyo ni vya Kusenyi, Kwikerege, Kwikuba, Makojo, Mkirira, Mmahare, Rukuba, Seka, Saragana, Kiemba, Kastam, Kiriba na Bulinga. Profesa Muhongo alivitaja vijiji vingine ambavyo vikundi vyake vitafaidika ni Bwai Kumusoma, Kigera Etuma, Bwai Kwitururu, Bugunda, Buira, Bujaga, Busamba, Busungu, Bwasi na Kasoma.

“Hii itakuwa ni mara ya tatu kugawa majembe ya kukokotwa na ng’ombe kwa vikundi vya wakulima, kwani kwa mara ya kwanza nilifanya hivyo wakati wa Sikukuu ya Krismasi mwaka jana,” alisema Muhongo na kuongeza kuwa katika sikukuu hiyo aligawa majembe 20, kisha wakati wa Sikukuu ya Pasaka mwaka huu akagawa majembe 25 na sasa anajiandaa kugawa mengine 40 katika kipindi cha Sikukuu ya Idd Elfitr.

“Tuna mkakati wa kuwaondoa wakulima kwenye jembe la mkono ili wote watumie plau, ndiyo maana ninajitahidi kuhamasisha mkakati huo kwa kutoa majembe hayo ili uwe mfano,” alisema.

Wakati huo huo, Profesa Muhongo alisema amechangia Sh milioni 12 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Chama Ch Mapinduzi (CCM) ya wilaya ya Musoma inayojengwa katika Kijiji cha Murang “Baadhi ya matumizi ya fedha hizo ni kulipia mafundi, ununuzi wa mifuko 200 ya saruji, kulipia gharama za ufyatuaji wa matofali, umwagiliaji wa maji na mambo mengine ya msingi ili kufanikisha ujenzi huo,” alisema.

Aidha, mbunge huyo alisema, kuna mambo mengi ya maendeleo yanayoendelea jimboni mwake ikiwamo kuanzisha matawi ya benki kwa ajili ya kutoa huduma za fedha kwa wananchi. Alisema, tayari benki za CRDB na NMB zina mawakala wanaotoa huduma ndani ya vijiji na kwamba hiyo ni hatua muhimu inayofanywa kabla ya ujenzi

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema tangu awe Waziri hajawahi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi