loader
Picha

Bunge laridhia Azimio la mafunzo wafanyakazi vyombo vya uvuvi

BUNGE limeridhia Azimio la Mkataba wa Kimataifa la Viwango vya Mafunzo na Utoaji Vyeti kwa Wafanyakazi wa Vyombo vya Uvuvi, ambalo linawapa fursa za ajira za ndani na za kimataifa wataalamu wa vyombo vya ndani vya uvuvi wakiwemo manahodha, maofi sa, wahandisi wa meli, maofi sa wa mawasiliano pamoja na wavuvi.

Azimio la Mkataba wa Kimataifa wa Viwango vya Mafunzo na Utoaji Vyeti kwa Wafanyakazi wa Vyombo vya Uvuvi wa mwaka 1995 (STCWF95), limewasilishwa Bungeni juzi na Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe.

Dk Kalemani alisema kuridhia mkataba huo, kunatoa nafasi ya kuwapo kwa wakaguzi na waangalizi wenye weledi, ambapo kuwepo kwao kutahakikisha matumizi endelevu ya rasilimali za bahari.

“Pia kunaimarisha vyuo vya ndani vya mafunzo ya uvuvi na kutambulika kimataifa na kuwepo kwa viwango bora vya ufundishaji wa wanafunzi katika vyuo vya uvuvi nchini,” alisema Dk Kalemani.

Alisema pia kunaimarisha usalama wa wafanyakazi katika vyombo vya uvuvi na hivyo kupunguza ajali na kuimarika kwa ulinzi, usalama na uhifadhi wa mazingira ya bahari pamoja na kuimarika kwa upatikanaji wa takwimu na taarifa mbalimbali katika sekta ya uvuvi.

Dk Kalemani alisema kupitishwa kwa mkataba huo, kutawezesha Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi, kutoa mafunzo na vyeti vinavyotambulika kimataifa katika uvuvi wa vyombo vya bahari kuu.

“Vyuo vilivyoko chini ya Wakala hapa nchini ni Bagamoyo (Pwani), Nyegezi (Mwanza), Kibirizi (Kigoma), Rorya (Mara) na Mikindani (Mtwara),” alisema.

Alisema kuridhiwa kwa mkataba huo kutawezesha vyuo vya mafunzo vyenye ithibati ya kutoa elimu ya mafunzo ya uvuvi yenye viwango vya kimataifa, kutayarisha wataalamu wenye weledi, watakaotumia vyombo vilivyo salama na kufanya shughuli za uvuvi kihalali.

Pia itawezesha kuwepo kwa viwango bora vya ufundishaji wanafunzi katika vyuo vya uvuvi nchini na kuimarisha usalama wa wafanyakazi katika vyombo vya uvuvi na hivyo kupunguza ajali.

Pia kuwepo kwa wakaguzi na waangalizi wenye weledi, ambao kuwepo kwao kutahakikisha matumizi endelevu ya rasilimali za bahari na kutaimarisha vyuo vya ndani vya mafunzo ya uvuvi na kutambulika kimataifa.

Dk Kalemani alisema azimio hilo linalenga kuweka, kusimamia na kudhibiti viwango vya kimataifa vya mafunzo na utoaji vyeti kwa wafanyakazi katika vyombo vya uvuvi, vyenye urefu wa kuanzia mita 24 na zaidi, vinavyotumika katika shughuli za uvuvi kwenye maji ya ndani na nje ya mipaka ya nchi.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema tangu awe Waziri hajawahi ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi