loader
WHO kuanzisha mfuko kusaidia shirika hilo

WHO kuanzisha mfuko kusaidia shirika hilo

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Ghebreyesus, ametangaza kuanzishwa mfuko wa kusaidia shirika hilo.

Kiongozi huyo jana alisema mfuko huo utahimiza watu na kampuni kuchangia fedha na kupanua msingi wa ufadhili kwa shirika hilo ili kupata fedha endelevu kwa ajili ya kusaidia changamoto mbalimbali za kiafya duniani.

Mfuko huo pia utatoa uungaji mkono wa kifedha kwa WHO na washirika wake kwa ajili ya kutatua changamoto za afya ya umma duniani, kukidhi mahitaji ya afya na kutimiza lengo la mpango wa kimkakati wa miaka mitano wa shirika hilo.

Katika hatua nyingine, shirika hilo limezishukuru nchi zinazoendelea kutoa uzoefu kuhusu njia za kufuatilia watu waliokuwa karibu na wagonjwa wacovid- 19, ambazo ni msingi wa ulinzi wa afya na ni mbinu muhimu ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa huo hasa kabla ya chanjo kupatikana.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7c41b2782edc081f6e8bb86393fae0ee.jpg

Marekani na Umoja wa mataifa zimelaani vikali mauaji ...

foto
Mwandishi: GENEVA, Uswisi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi