loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Liverpool kukabidhiwa taji uwanja huru

MCHEZO ambao Liverpool inaweza kukabidhiwa taji la Ligi Kuu England utafanyika katika uwanja huru, umesema uongozi wa kitaifa wa mpira wa miguu.

Naibu Mkuu wa Idara hiyo, Robert Roberts alisema mechi sita zinaweza kuhamishwa kutokana na ombi la polisi. Hii ni pamoja na mchezo wa watani wa jadi wa Merseyside, Manchester City dhidi ya Liverpool.

Roberts alisema majadiliano na Ligi Kuu yalikuwa mazuri na yalilenga kuzingatia kipaumbele cha afya ya umma. Ligi Kuu imepangwa kuanza tena Juni 17, chini ya idhini ya serikali.

Mechi ambazo zinaweza kuhamishiwa katika uwanja huru ni: Manchester City v Liverpool, Manchester City v Newcastle, Manchester United v Sheffield United, Newcastle v Liverpool na Everton v Liverpool mchezo ambao Liverpool atakabidhiwa kombe.

“Tumefikia makubaliano ambayo yanasawazisha mahitaji ya mpira wa miguu, huku pia tukipunguza mahitaji ya polisi,” alisema Roberts.

“Mechi nyingi zilizobaki zitachezwa, nyumbani na ugenini kama ilivyopangwa, na idadi ndogo ya marekebisho itafanyika na mechi ambazo zitachezwa katika viwanja huru, na ripoti kadhaa bado hazijakubaliwa.

“Mpango huu utaendelea kila wakati ili kuhakikisha afya ya umma na usalama na sehemu muhimu ya hii ni kwa mashabiki kuendelea kuheshimu umbali wa mita moja, na siyo kuhudhuria au kukusanyika nje ya uwanja.”

Liverpool, inatarajiwa kuchukua taji lao baada ya miaka 30, ikiwa inaongoza Ligi Kuu kwa alama 25 na ina michezo tisa iliyobaki, na timu hiyo inayonolewa na Jurgen Klopp inaweza kukabidhiwa taji katika mchezo dhidi ya wapinzani wao Everton.

Polisi wa Merseyside wanasema “kuhusiana na uhalifu na machafuko haina pingamizi kwa mchezo huo kuchezwa Goodison Park, na itakuwa tayari kutoa chochote kinachohitajika kutoka kwetu,”.

Lakini konstebo, Rob Carden aliongeza: “Maamuzi yanayohusiana na hatari ya afya ya umma yanafanywa na Serikali na mamlaka ya Afya ya Umma ya England.

“Uamuzi wa mwisho unakaa na mamlaka ya ushauri ya usalama ambayo inaongozwa na Halmashauri ya Jiji la Liverpool sambamba na maamuzi yaliyotolewa kitaifa kuhusiana na hafla za michezo.”

Ligi Kuu ilisema “matarajio yake ni kukamilisha ratiba yote ya msimu huu nyumbani na ugenini, inapowezekana”.

Iliongeza: “Tunafanya kazi na klabu zetu kuhakikisha kuwa hatari zinapimwa na kupunguzwa, tukishirikiana na polisi katika ngazi ya chini na kitaifa.

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi