loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JPM ang’ara uongozi Afrika

UTENDAJI kazi wa Rais John Magufuli, umeendelea kutambulika kimataifa, baada ya kutajwa kuwa ni miongoni mwa watu 10 barani Afrika wakiwemo viongozi, wanaotambulika kwa kuleta mabadiliko makubwa.

Jarida la ‘The Africa Report’ la hivi karibuni, lilisema watu hao 10 akiwemo Rais Magufuli, ni kati ya watu 50 wa Afrika, waliofanya mabadiliko makubwa.

Lilisema Rais Magufuli amefanikiwa kufanya mapinduzi makubwa katika uendeshaji wa miradi ya uchumi na huduma za kijamii katika kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano.

Hatua hizo zimesababisha uchumi wa Tanzania, kukua na kuwa miongoni mwa uchumi unaokua kwa kasi barani Afrika. Ripoti hiyo ilitaja mambo kadhaa, yaliyofanywa na Rais Magufuli kwenye utawala wake katika kipindi cha miaka mitano, kuwa ni pamoja na kuleta mabadiliko makubwa kwenye utumishi wa umma, kwa kurejesha nidhamu ya kazi, kuziba mianya ya ukwepaji kodi na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma.

Sambamba na hilo, pia Rais Magufuli ni kiongozi aliyeweka mazingira mazuri ya kufanya biashara nchini Tanzania. Pia ripoti hiyo inasema Rais Magufuli amekuwa kiongozi wa mfano, ambapo baada ya kuingia madarakani mwaka 2015, alipunguza kiwango cha mshahara wake kutoka Dola za Marekani 15,000 hadi Dola za Marekani 4,000 kwa mwezi.

Jarida hilo linasema Rais Magufuli ametumia vema misaada ya maendeleo kutoka Serikali ya China kwa ajili kuboresha miundombinu, ikiwemo barabara na reli. Linasema tangu alipoingia madarakani, Magufuli amekuwa akipunguza utegemezi wa fedha za wahisani kutoka nje, ambapo kwa mwaka wa fedha 2016/17 kodi mbalimbali zilianzishwa, kama njia ya kuongeza makusanyo ya kodi, kwa ajili ya kupafa fedha za miradi ya maendeleo.

Aidha, Tanzania imeanza kufaidika na sekta ya madini, baada ya Sheria ya Madini kufanyiwa marekebisho, na hivi sasa sekta hiyo inachangia pato la taifa kwa asilimia 5 kutoka asilimia 4.8 ya mwaka 2018/19. Katika hilo, kodi mbalimbali za madini, ambazo awali wafanyabiashara walikuwa wakikwepa kulipa, hivi sasa zinalipwa.

Hata wale waliokuwa wakifanya biashara za magendo, kwa kusafirisha nje madini kwa kukwepa kodi, kwa sasa mianya hiyo imezibwa. Suala lingine linaloonesha Rais Magufuli amefanya mambo ya msingi yanayoonekana kimataifa, ni jinsi alivyoweza kupunguza utegemezi wa bajeti kutoka kwa wahisani, ambapo kwa mwaka wa fedha 2020/21 utegemezi wa wahisani ni Sh bilioni 138.32 wakati mwaka 2016/17 utegemezi ulikuwa Sh bilioni 483.

Jarida hilo linaeleza kuwa lengo la kufanya uchambuzi huo na kuja na ripoti hiyo, ni kuangalia wanawake na wanaume wa Afrika, ambao wamefanya jambo au mambo yenye kuleta mabadiliko makubwa kwenye jamii, kiasi cha kufanya maamuzi yao yazue gumzo. Ripoti hiyo hutumia vigezo vitatu vikubwa, kuamua watu wanaopaswa kuingia kwenye orodha ya watu 50 waliozua Gumzo Barani Afrika, kutokana na uamuzi au kazi zao kwa jamii.

Moja ya vigezo hivyo ni ubunifu, hatua za kubadilisha hali na usimamizi wa hatua, zilizochukuliwa kuleta ufanisi katika maamuzi. Vigezo hivyo vimetumika kuonesha jinsi mawazo mapya, yanavyoweza kuleta mabadiliko ya mtazamo na kuhusisha jamii kubwa.

Baadhi ya watu wengine walioingia kwenye orodha hiyo ya waliosababisha Gumzo Barani Afrika ni Mshindi ya Tuzo ya Nobel mwaka 2019, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, Mfanyabiashara maarufu na mwanamageuzi mashuhuri nchini Nigeria, Aliko Dangote, Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo na Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Ahmed wa Ethiopia ndiye anayeongoza kwenye orodha hiyo, kwa kusababisha mabadiliko chanya nchini mwake, kwa kuwa mwanadiplomasia aliyemaliza mgogoro baina ya Ethiopia na nchi jirani ya Eritrea. Nafasi ya 10 imeshikwa na Julius Malema, ambaye ni kiongozi wa upinzani nchini Afrika Kusini.

TRAFIKI Kanda Maalum Dar es Salaam imese- ma ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi