loader
Uganda yaahirisha kufungua shule

Uganda yaahirisha kufungua shule

SERIKALI ya Uganda imeahirisha kufungua shule kwa mwezi mmoja zaidi kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho. Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni, alisema kufungua shule ilikuwa hatari, kwa sababu hakukuwa na vifaa vya kutosha vya kuwapima wanafunzi kila baada ya wiki mbili.

Rais Museveni alisema kila kijiji, kitapewa televisheni mbili ili kuwezesha wanafunzi kufuatilia masomo wakiwa majumbani. Kuhusu waendeshaji wa usafiri wa umma, alisema wameruhusiwa kuanza lakini iwe nusu ya uwezo wao.

Alisema usafiri wa pikipiki umeruhusiwa kubeba mizigo tu na siyo abiria. Nyumba za ibada ikiwemo makanisa na misikiti, sehemu za starehe, baa na maeneo ya michezo, yataendelea kufungwa kwa siku 21 na maduka makubwa yameruhusiwa kufunguliwa kwa masharti ya kuhakikisha wateja wao, wanazingatia umbali kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Imeelezwa kuwa watu wataanza kugawiwa barakoa, zinazotolewa na serikali.

Rais alisisitiza kuwa wale wasiokuwa na barakoa, wabaki nyumbani. Pia Rais Museveni aliagiza mashitaka ya jinai 4,000 ya watu waliokamatwa kwa kukiuka amri ya kubaki nyumbani iliyotolewa mwanzoni, yapitiwe upya.

Aliagiza kuwa wale watakaobainika kuwa na kesi ndogo za kujibu, waachiwe huru. Alisema serikali itaendelea na mpango wake wa kugawa chakula kwa watu masikini.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8aab5fce300e66d467095bbe216372b8.jpg

Marekani na Umoja wa mataifa zimelaani vikali mauaji ...

foto
Mwandishi: KAMPALA, Uganda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi