loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kasi ya JPM yavuta viongozi duniani kuja kujifunza

TANZANIA inatarajia kupokea idadi kubwa ya viongozi wa serikali mbalimbali duniani, ambao watakuja kujifunza utekelezaji na usimamizi wa miradi unaofanywa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, mkoani Kigoma jana, wakati akizindua barabara za kiwango cha lami iliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.

Alisema utekelezaji na usimamizi wa miradi unaofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli, umezikosha nchi nyingi duniani, jambo linalofanya nchi hizo kutaka kuja kujifunza namna Tanzania inavyoitekeleza na kuleta mabadiliko makubwa.

“Utekelezaji wa mradi wa barabara za kiwango cha lami katika Manispaa ya Kigoma chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia ni miongoni mwa miradi iliyotekelezwa kwa kufuata maelekezo ya serikali ambayo umeleta heshima kubwa katika nidhamu ya utekelezaji na usimamizi wa fedha,” alisema.

Jafo alisema utekelezaji wa mradi huo ni sehemu ya miradi iliyopo kwenye halmashauri za manispaa na majiji manane nchini.

“Ipo miradi mingine inatekelezwa katika halmashauri 18 nchini, ikiwa na thamani ya Sh bilioni 200, ambayo ni ujenzi wa barabara za lami za kiwango cha juu,” alisema.

Awali, Meneja wa mradi wa ujenzi wa barabara za kiwango cha lami katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Wilfred Shimba, alisema kiasi cha Sh bilioni 21 kimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo, ambapo barabara za lami zenye urefu wa kilometa 12.1 zimejengwa na mifereji miwili.

Alisema barabara hizo zimekamilika zikiwa chini ya uangalizi wa mkandarasi kwa mwaka mmoja na kiasi cha Sh bilioni 17 kimeshalipwa kwa mkandarasi kampuni ya China Railways 15 Group na kiasi cha Sh bilioni 1.1 kimeokolewa katika kupunguza gharama.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Emanuel Maganga, alisema barabara za lami katika Manispaa ya Kigoma Ujiji zimebadilisha sura ya mji huo na zimekuwa chachu ya shughuli za maendeleo katika mji huo ambao ndiyo makao makuu ya mkoa.

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wakazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kurekebisha na kuboresha nyumba zao kulingana na maboresho ya miundombinu na uboreshaji miji unaofanywa na serikali.

Naye, Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji anayetokana na Chama Cha ACT Wazalendo, Huswein Ruhava, alisema kama kuna mtu anapaswa kupongezwa kwa utekelezaji wa mradi huo, ni Waziri Jaffo na Mtangulizi wake, George Simbachawene, ambao walisimamia kidete kuhakikisha fedha za utekekezaji wa mradi huo zinapatikana na mradi unatekelezwa.

TRAFIKI Kanda Maalum Dar es Salaam imese- ma ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi