loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ligi Kuu Zanzibar bila mashabiki

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetangaza kwamba Ligi Kuu ya Zanzibar itachezwa katika kituo kimoja tena bila mashabiki, ikiwa njia moja ya kudhibiti maambukizi ya maradhi ya Covid-19.

Hayo yamethibitishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Omar Hassan Omar ‘King’ alipokuwa akisoma muongozo wa kiafya uliotolewa na Serikali baada ya kurhuhusu ligi hiyo kuendelea . King alisema kuwa hatua hiyo inalenga pia kuepusha timu kusafiri na kwa kuzingatia hasa hali ya maradhi pia kupunguza baadhi ya gharama.

Kituo kitakachotumika kwa ajili ya ligi hiyo ni cha Unguja pekee kwa sababu kuna viwanja vya kutosha sambamba na kuangalia uwiano wa timu ambazo zipo Pemba na Unguja. King alisema kuwa kwa mujibu wa idadi ya timu hizo, Unguja kuna timu 11 na Pemba timu tano, ambazo ni rahisi kuzisafirisha tofauti na Unguja ambapo maambukizi yanakuwa mengi zaidi.

Hata hivyo alisema kuwa katika hatua ya awali ligi yao itakapoanza haitaruhusu mashabiki kuingia uwanjani wakati wa mechi au mazoezi na watalazimika kuangalia na kusikiliza katika televisheni na radio.

Hivyo alisema wahusika wote wanapaswa kuzingatia taratibu za kiafya kuanzia mazingira ya viwanja pamoja na huduma muhimu za wafanyakazi wa uwanja, wachezaji, waamuzi, viongozi wa klabu pamoja na watu wote watakaokuwepo uwanjani.

Aidha alieleza Serikali iliagiza Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Michezo (BTMZ), ZFF pamoja na wadau wa michezo ikiwemo klabu iandae miongozo na utaratibu uliobora kwa kushirikisha kikamilifu na Wizara ya Afya ili kuweka miongozo ya kiafya.

Alisema utaratibu huo unalenga kusaidia kuwepo kwa mazingira wezeshi na salama ili kuendelea na michezo na kuepusha kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wametajwa katika tetesi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi