loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Chelsea yamuwania Timo Werner

CHELSEA iko kwenye mazungumzo ya kusaini mshambuliaji wa RB Leipzig, Timo Werner. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 24 alihusishwa kutakiwa na Liverpool na kusema aliona fahari. Lakini BBC Sport inaelewa Liverpool haina nia ya kumsaini Werner, ambaye amefunga mabao 25 msimu huu.

Ripoti zinaonesha kuwa thamani yake ni karibu Paundi milioni 54. Mwezi uliopita, mshambuliaji wa Ufaransa, Olivier Giroud aliongeza mkataba wake kwa mwaka kusalia Stamford Bridge. Werner, ambaye amecheka na nyavu mara 11 katika michezo 29 ya timu ya Taifa ya Ujerumani, angekuwa mchezaji wa pili kusaini Chelsea kwa msimu ujao baada ya kukamilisha mpango wa kumsajili Hakim Ziyech kutoka Ajax kwa pauni milioni 37 mwezi Februari.

Aliivutia Leipzig kufuatia uhamishaji wake wa mwaka 2016 kutoka klabu ya nyumbani kwao ya Stuttgart. Werner alifunga ‘hattrick’ katika ushindi wa 5-0 wa Leipzig dhidi ya Mainz na pia akacheka na nyavu mara tatu dhidi ya wapinzani hao katika ushindi wa 8-0 kabla ya Krismasi.

Januari, Kocha Mkuu wa Chelsea, Frank Lampard alihusishwa na Paris St- Germain na mshambuliaji Edinson Cavani na Dries Mertens wa Napoli lakini hawakufanikiwa.

MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich, Robert Lewandowski, amesema anadhani kocha wa ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi