loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Msigwa aomba kugombea urais

MBUNGE wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (CHADEMA) amejitosa kwenye kinyang’anyiro kuwania kuteuliwa na chama chake kuwa mgombea nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Msigwa ni mwanachama wa pili cha chama hicho, kuonesha nia ya kutaka kugombea nafasi ya urais, ikiwa ni siku chache baada ya aliyewahi kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kutangaza nia hiyo akiwa ughaibuni.

Aidha, jana jioni aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya Awamu ya Nne ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Kanda ya Kati wa Chadema, Lazaro Nyalandu alitarajiwa kutangaza nia kama hiyo. Akitangaza nia yake jijini hapa jana, Msigwa alisema:

“kama nilivyodokeza siku zilizopita, leo natangaza nia ya kugombea nafasi ya Rais na tayari kwa mujibu wa Katiba ya chama nimewasilisha rasmi taarifa ya kuomba chama kiniteue kugombea nafasi ya urais.”

Alisema jambo moja la msingi, lililomsukuma kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi katika nchi ni kutaka kuongoza mageuzi makubwa ya kiutawala, kiuchumi na kielimu, yatakayoleta maendeleo makubwa na ya haraka, yaliyo jumuishi na endelevu kwa manufaa ya sasa na ya tanzania ijayo.

Alisema kiongozi bora huwa na maono na ndoto ya nchi anayotaka kuijenga, hivyo ndoto yake ni kuitoa Tanzania katika orodha ya nchi maskini sana duniani na kuipa mwelekeo sahihi wa kifikra, kiutawala na kisera, utakaoiwezesha kuja kuwa miongoni mwa nchi zenye maendeleo makubwa kabisa duniani.

“Ninayo dhamira ya kweli, maono sahihi na uwezo wa kutosha wa kuiongoza vema Tanzania ili kuifikia ndoto hii kubwa. Naam, ndoto ya Tanzania yenye maendeleo ya uhakika,” alisema Mchungaji Msigwa.

Msigwa alisema kutaka kuwania nafasi hiyo, hamaniishi kuwa utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) haujafanya kitu, lakini bado imeendelea kusuasua kimaendeleo kwa muda mrefu na kupoteza mwelekeo na kushindwa kabisa kupiga hatua kubwa na mpya za kimaendeleo.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi