loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Magufuli- Kagombane na mkeo

Rais DK John Magufuli ametengua uteuzi wa viongozi wakuu Mkoa wa Arusha kwa sababu kwa takribani miaka miwili walikuwa wanagombana.

Ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kumuapisha Idd Kimanta kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na pia kushuhudia viapo vya wakuu watatu wa Wilaya.

“Kila mmoja ni bosi, kila mmoja anatengeneza mizengwe ya mwenzake, sikufurahishwa. Walifanya kazi zao lakini waliniudhi wao kutokushirikiana na kufanya yale ambayo nimewaagiza…sasa kama wanakwenda kubishana wakabishanie hukohuko uraiani lakini ndani ya Serikali ninayoiongoza hapana

‘…lakini hii iwe fundisho kwa viongozi ninaowateua. Ni lazima tujenge element za kuvumiliana. Kama ni kubishana na kugombana kabishane na mkeo wako na watoto wako lakini ndani ya Serikali ninayoiongoza hapana. Ni lazima tujifunze kuzingatia sheria na maadili, na viapo vyetu tunavyoviapa “amesema Rais.

Pia amesema aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alikuwa chanzo cha mgogoro wa ardhi kati ya Jiji la Arusha na msikiti jijini humo kwa kutosema ukweli ili asionekane mbaya.

“Lengo ni kuonekana yeye ni mzuri sana, kila mmoja ni kutoa ahadi, tusitoe ahadi ambazo haziwezekani. Ni lazima tusimamie sheria” amesema Rais.

Amewaeleza viongozi wapya wa Arusha kuwa hataki hayo yakajitokeze, wavumiliane na washirikiane.

“Kwa hiyo nachowaomba kafanyeni kazi, na ikiwezekana mkaridhike na mlichonacho…sana mkaridhike na kazi mliyonayo, mkawatumikie Watanzania. Ninawaamini vijana, ninawaamini wazee, ninawaamini wakina mama, ninawaamini everybody (kila mtu), kikubwa mkafanye kazi zenu mlizopangwa” amesema.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi