loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

EAC yatajwa kuwa bora Afrika, ya pili duniani

JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC) imetajwa kuwa ndiyo jumuiya bora iliyounganika baina ya nchi wanachama kuliko jumuiya nyingine yoyote ya maendeleo katika bara la Afrika.

Aidha, katika ripoti ya mwaka 2018 imeitaja jumuiya hiyo kuwa ya pili kwa ubora duniani, ikitanguliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya (EU). Ripoti ya Maendeleo ya Jumuiya za Afrika (ARII) toleo la mwaka 2019, iliyotolewa hivi karibuni, ilisema EAC imeshika nafasi ya kwanza kati ya jumuiya nane za Maendeleo za Afrika zinazotambuliwa na Umoja wa Afrika (AU).

ARII ni chombo kinachoainisha namna nchi zinazounda jumuiya zinavyopiga hatua za maendeleo hasa katika kuimarisha uchumi na mshikamano baina ya nchi wanachama au nchi moja moja. Jumuiya za maendeleo barani Afrika zinazotambuliwa na Umoja wa Afrika zilizoingizwa katika kinyang’anyiro hicho ni EAC, Umoja wa Nchi za Kiarabu Magharibi mwa Afrika (AMU) na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati (ECCAS).

Nyingine ni Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Pembe ya Afrika (IGAD), Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas), Jumuiya ya Nchi za Sahel na Sahara (CENSAD), Jumuiya ya Soko la Pamoja Mashariki na Kusini mwa Afrika (Comesa) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Miongoni mwa vigezo vilivyoangaliwa ni pamoja na uhuru wa kutembea baina ya wananchi wa nchi wanachama, muunganiko wa miundombinu, maendeleo ya biashara ndogondogo, uzalishaji wa pamoja na biashara za pamoja ndani ya jumuiya.

Kwa kuzingatia vigezo hivyo, Jumuiya ya Afrika Mashariki imepata alama za juu kuliko jumuiya nyingine yoyote barani Afrika. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, EAC imepata wastani mzuri wa alama 0.537, ikifuatiwa na AMU alama 0.488, ECCAS alama 0.442 na IDAD alama 0.438.

Nyingine ni Ecowas alama 0.425, CAN-SAD alama 0.377, Comesa alama 0.367 na SADC alama 0.337. Akizungumzia ripoti hiyo jana, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Liberate Mfumukeko, alieleza kufurahishwa na matokeo hayo. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa EAC kuzipiku jumuiya ningine barani Afrika.

TRAFIKI Kanda Maalum Dar es Salaam imese- ma ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

1 Comments

  • avatar
    Francis
    26/06/2020

    Hii ni habari Nzuri sana nimefurahi Kunioa habari hiikwa kuzingatia mimi ni mwanafunzi nchi ni japani nikitokea Tanzania ninasomea mahusiano ya Kimata Nitafurahi kama nikipata report za regional economic integration hasa report zilizopita natazamia kuangalia changamoto zinazozikabili regional integration

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi