loader
Trump aongeza muda viza, wafanyakazi wageni

Trump aongeza muda viza, wafanyakazi wageni

RAIS wa Marekani, Donald Trump ameongeza muda wa viza za bahati nasibu na wafanyakazi wa kigeni kusitishwa hadi mwisho wa mwaka.

Wafanyakazi wenye ujuzi mkubwa wa kiufundi, wasio katika sekta ya kilimo na maofisa wakuu wa kampuni wataathirika zaidi na hatua hiyo.

Ikulu ya Marekani imesema hatua hiyo itaibua ajira kwa Wamarekani walioathirika kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (covid 19).

Hata hivyo, wakosoaji wanasema Ikulu hiyo ya Marekani inatumia janga la corona ili kuweka masharti magumu kwenye sheria za uhamiaji. Katika mkutano na waandishi wa habari, Rais alisema usitishwaji utakaoendelea hadi mwisho wa mwaka huu utawaathiri watu 525,000.

Watu 170,000 walizuiliwa na hatua ya kusitisha viza za bahati nasibu ambazo zinawapatia raia wa kigeni makazi ya kudumu nchini Marekani. Ikulu ya Marekani mara ya kwanza ilitangaza kwamba ilikuwa inasitisha viza hizo mwezi Aprili agizo ambalo lilitarajiwa kukamilika juzi.

Hata hivyo, raia wa kigeni walio na viza sasa hawataathirika kutokana na sheria hizo mpya.

Agizo hilo pia litawashirikisha wale walio na viza H-1B, ambazo nyingi hupewa wafanyakazi wa Kihindi ambao wana ujuzi wa kiufundi. Wakosoaji wanasema viza hizo zimeruhusu kampuni za teknolojia za Silicon Valley kuwapa kazi wageni wanaolipwa mishahara midogo.

Mwaka uliopita, kulikuwa na watu 225,000 waliotuma maombi wakishindania kazi 85,000 zilizopo kupitia mpango wa viza za H1-B.

Agizo hilo litasitisha kwa muda viza nyingi aina ya H-2B kwa wafanyakazi wa msimu walio sekta ya utalii isipokuwa wale wa kilimo, viwanda vya chakula na wataalamu wa afya.

Agizo hilo pia litawaathiri wale wanaotaka viza za muda mfupi za J-1, orodha inayowashirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu na wafanyakazi wa ndani.

Maprofesa na wasomi wengine hawakuguswa na agizo hilo. Kutakuwa na kifungu kuwaruhusu baadhi ya walioathiriwa wakituma maombi.

Viza za mameneja na wafanyakazi wengine muhimu wa kampuni za kimataifa zitasitishwa.

‘’Hatua hii imewalenga watu bora na werevu na wenye thamani kwa uchumi wa Marekani,” alisema afisa mmoja mkuu kwa njia ya simu.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Masomo ya Uhamiaji, Mark Krikorian, ambaye taasisi yake iliunga mkono sheria kali za uhamiaji, alisema hatua hiyo ni muhimu iliyotekelezwa na utawala wa Trump ili kulinda kazi za raia wa Marekani.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5f393b02b8cec6f42eeecba769753a02.jpg

Marekani na Umoja wa mataifa zimelaani vikali mauaji ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi