loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Corona igeuzwe fursa kuendeleza elimu

HIVI karibuni Shirika la Hakielimu lilikuwa na mjadala wa kutafakari mfumo wa elimu ya Tanzania, unavyotumia athari hasi za Covid-19 kama fursa za kuboresha elimu katika kuadhimisha Siku ya Mtoto Afrika Juni 16.

Sekta ya elimu kama nyingine imepitia kipindi kigumu kutokana na maambukizi ya virusi vya corona (Covid-19), kuvuruga na kuathiri sehemu kubwa ya utoaji wa elimu duniani kote.

Kwa mujibu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (Unesco), takribani wanafunzi bilioni 1.54 wakiwemo watoto wa kike milioni 743 hawako shuleni, hivyo kuwa katika hatari ya kukosa haki yao ya kujifunza na kupata elimu rasmi ipasavyo. Nchini Tanzania, Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto na Wanawake (UNICEF) lilisema zaidi ya watoto milioni mbili wa umri wa shule ya msingi na watoto milioni 1.5 wa umri wa shule za sekondari hawako shuleni.

Hivyo Hakielimu imeishauri serikali kuendeleza mijadala zaidi juu ya upatikanaji wa elimu ya watoto kipindi hiki cha maambukizi ya Covid – 19 na hata baada ya maambukizi hayo kuisha.

Hii ni pamoja na kuwa na mipango kusaidia serikali, kufidia ombwe la watoto kujifunza lililochangiwa na kufungwa taasisi za elimu. Ni vema kuzitumia changamoto zilizotokana na janga la corona, kama fursa kujifunza njia bora ya kuimarisha mfumo wa elimu nchini, uwe nyumbufu na unaokidhi matakwa ya utoaji elimu na unaoendana na mahitaji ya karne ya 21.

Pia ni bora kuwekeza zaidi katika matumizi ya teknolojia katika utoaji elimu kwa watoto juu ya namna ya shule zinavyoweza kutumia teknolojia zaidi, kusambaza maarifa yanaoyokusudiwa. Changamoto ya Covid -19 igeuzwe kuwa fursa ya mabadiliko katika namna inavyowekezwa katika uendeshaji wa shule na taasisi za elimu nchini.

Kwa kuwa nchini kuna upungufu mkubwa wa miundombinu ya Tehama, ambayo ingeweza kurahisisha ujifunzaji, changamoto ya Covid-19 inapaswa kuwa ni fursa ya kutafakari namna ambayo inawezekana kuimarisha mifumo ya ulinzi wa mtoto awapo shuleni au nyumbani.

Hii inaweza kuanza na kuhusisha elimu ya teknolojia, elimu ya awali na kuendesha vipindi vya kuwajengea uwezo wazazi, walezi, walimu na kuhamasisha juu ya matumizi ya teknolojia.

Pia Covid-19 iwe fursa ya kuwafikia watoto ambao awali hawakuwa shuleni, kwa kuwa kulikuwa na njia mbadala zilizopendekezwa za wanafunzi kujifunza katika kipindi cha hicho. Njia hizo zinaweza kutumiwa kuwafikia watoto na makundi ya watoto, walio nje ya mfumo wa shule na waishio katika mazingira magumu.

SERIKALI ya Rais John Magufuli tangu ilipoingia madarakani mwaka 2015, ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

1 Comments

  • avatar
    Comfort 2020 Comfort
    03/07/2020

    Kazi yako nzuri na nilishawahi kufanya iliishia hapa 1. Kuandaa TOFAUTI 2. Kuandaa Tofari 3. Kuona 4. Kusikia 5. KUONYESHA N.K

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi