loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Utafutwe mwarobaini mgogoro Bandari ya Bagamoyo

KWA zaidi ya wiki sasa wafanyabiashara wanaotumia Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani, wameisusa na matokeo yake ni kushuka kwa kasi kwa mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, ambayo kitovu chake cha uchumi ni bandari hiyo.

Mgogoro huo una sura tofauti, ambapo ndani yake kuna hofu ya kutaka kufanya biashara kwa misingi ya ukwepaji kodi stahiki. Lakini, pia kuna baadhi ya madai ya kutokuwepo kwa huduma nzuri kutoka kwa baadhi ya watendaji wa mamlaka bandarini.

Siku chache zilizopita, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa alisema kwa mwezi, wilaya hiyo ambayo inategemea bandari hiyo kama kitovu cha uchumi wa Bagamoyo, ilikuwa ikikusanya mapato Sh bilioni 2.6, lakini mwezi huu imekusanya Sh milioni 293 tu kutokana na kufukuta kwa mgogoro huo.

Mgogoro huo ambao ulianza miaka ya nyuma, baada ya serikali kuanza kuzuia bandari bubu, zilizotawala eneo hilo na hivyo serikali kukosa mapato huku wafanyabiashara wakijunufaisha.

Lakini pia ukosefu wa elimu ya mlipa kodi na ukosefu wa baadhi ya mamlaka zinazopaswa kuwepo bandarini, kusimamia vizuri huduma za bandari ili wanaotumia walipe kodi stahiki .

Jambo jingine ni madai ya ukosefu wa huduma bora kwa baadhi ya watumishi wa mamlaka za serikali katika bandari hiyo kwa sasa, ambapo inadaiwa kuna nyakati wateja ambao ni wafanyabiashara na watoa huduma, wanajibizana na kufikia kupigana ofisini.

Sasa mchanganyiko wa haya yote, ndio umezaa tatizo linalosababisha uchumi kuyumba, wakati tofauti hizo zinawezwa kuzungumzwa na kutafutiwa suluhu ya kudumu ili maendeleo na uchumi wa nchi usiyumbishwe na baadhi ya watu wachache wasio waaminifu.

Kinachoonekana hapo bandarini ni kukosekana kwa utashi na maamuzi ya busara, kwani wafanyabiashara wao wanagoma kuleta mizigo, kwa madai kuwa wananyanyaswa na baadhi ya watoa huduma ili hali wanalipa kodi stahiki. Lakini, pia ndani ya madai hayo yapo yenye mashiko.

Lakini mengine ni janja ya baadhi yao ya kutaka kukwepa kodi, jambo ambalo baadhi yao wanasema wanatozwa ilivyo halali na hawapati faida.

Sasa basi ni vyema pande zote, zikae chini tutafuta suluhu na pia elimu itolewe kwa kiwango cha juu kwa wafanyabiashara hao, kwani yawezekana kuna ufanyaji biashara wa mazoea ya miaka ya 1950, wakati hivi leo sheria mbalimbali zikiwemo za tozo za kodi na nyinginezo, zinapaswa kufanya kazi.

SERIKALI ya Rais John Magufuli tangu ilipoingia madarakani mwaka 2015, ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi