loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwakyembe azindua kitabu kuenzi Serikali ya JPM

KITABU cha kihistoria kinachohimiza Watanzania kuwa wazalendo, kujitambua na kujitegemea kwa kuiga mfano wa Rais John Magufuli na Serikali yake aliyebomoa hekalu na kulijenga upya, kimezinduliwa.

Kitabu hicho chenye kichwa, ‘Rais Dk John Pombe Joseph Magufuli na Serikali yake Walivyobomoa Hekalu na Kulijenga Upya,’ kilizinduliwa jijini hapa hivi karibuni na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (pichani) kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni katika wizara hiyo, Dk Emmanuel Temu.

Akizindua kitabu hicho chenye sura 13 kurasa 290, kilichoandikwa na Mwalimu wa Masomo ya Kemia na Baolojia katika Shule ya Sekondari Viwandani jijini hapa, Projestus Kabagambe, Dk Mwakyembe alisema, kitabu hicho ni kumbukumbu kwa kizazi kijacho kuhusu utendaji bora wa Rais Magufuli na serikali yake.

“Kitabu hiki kinahimiza kuwapo kwa falsafa ya uzalendo, kujitambua na kujitegemea kwa Watanzania wote kwa kuiga mfano wa Rais Magufuli mzalendo namba moja,” alisema.

Alisema historia haifi, kupitia kitabu hicho historia ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano iliyofaulu kulibomoa hekalu na kulijenga upya kwa kufanya maboresho makubwa pamoja na kujenga miradi mikubwa ya kimkakati itasomwa na vizazi vijavyo kupitia kitabu hicho.

Waziri Mwakyembe alimpa kongole mtunzi wa kitabu hicho Mwalimu Kabagambe akasema historia ya nchi hii itamkumbuka kwamba aliweka kumbukumbu ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano katika maandishi kwa ajili ya watoto, wajukuu hata vitukuu.

Akizungumza mtunzi wa kitabu hicho, Mwalimu Kabagambe alisema, kimeandikwa kwa miaka minne na robo tangu Machi 2016 hadi Machi 2020, kimesheheni mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano na pia kimeshauri kuanzishwa kwa falsafa ya uzalendo, kujitambua na kujitegemea nchini.

Akitoa wasifu wa kitabu hicho, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John, Dk Elizabeth Msoka alisema, mtunzi ameandika kwa umahiri kuhusu kuvunja helaku la kulijenga kwa muda mfupi, akimaanisha kuondoa uozo mbalimbali uliokuwapo katika nchi kabla yake.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Dk Yahya Msigwa ambaye alipewa heshima kusahihisha kitabu hicho alisema, kitabu hicho kinazungumzia makubwa mengi ambayo tangu uhuru hayakufanyika.

“Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), mradi wa ujenzi wa umeme Rufiji na miradi mingine ambayo katika awamu zilizopita ilishindakana,” alisema Dk Msigwa.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi