loader
ZEC- Tumejipanga Uchaguzi Mkuu uwe huru

ZEC- Tumejipanga Uchaguzi Mkuu uwe huru

TUME ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imezindua Kamati ya Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi Namba 4 ya Mwaka 2018 itakayofanya kazi kwa kushirikiana na vyama vya siasa na taasisi nyingine kuona sheria za uchaguzi zinafuatwa na kupunguza malalamiko ya ukiukwaji wa sheria hizo.

Makamu Mwenyekiti wa ZEC, Mabrouk Jabu aliwataka wajumbe wa kamati hiyo kujipanga vizuri kuona masharti yote yaliyomo katika kamati hiyo yanafuatwa kwa lengo la kuona Uchaguzi Mkuu unakuwa huru na haki.

Jabu alisema ZEC imejipanga kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu unakuwa huru na haki na ndiyo maana kamati muhimu zinazotakiwa kuundwa katika uchaguzi huo zimeanza kuzinduliwa.

“Matarajio ya Tume ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 kuona Uchaguzi Mkuu unakuwa huru na haki na ndiyo maana kamati zinazotakiwa kuundwa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi zinazinduliwa kwa ajili ya kufanya kazi,” alisema Makamu Mwenyekiti wa ZEC.

Mapema Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Idaroud Faina alizitaja kamati zinazotarajiwa kuundwa kuelekea Uchaguzi Mkuu ni Fedha, Ununuzi na Usambazaji wa vifaa vya kupigia kura, Elimu na Ulinzi na Usalama wa vyombo vya dola.

“Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020 tunatakiwa kuunda kamati ambazo zitasimamia kwa karibu uchaguzi huo kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo vyama vya siasa na kamati za ulinzi...tayari tumefanikiwa kuunda kamati hizo na zipo tayari kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria za uchaguzi,” alisema Faina.

Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Hassan Nasir aliwaomba wananchi kuondoa hofu kuelekea Uchaguzi Mkuu huku akiwataka viongozi wa vyama vya siasa ambao ni wajumbe wa kamati hiyo kutii viapo vyao.

“Hii ni kamati muhimu ya ushauri kwa ajili ya kufuatilia maadili ya vyama vya siasa kuona Uchaguzi Mkuu unakuwa huru na haki na sisi vyombo vya ulinzi ikiwemo Jeshi la Polisi tumefurahishwa kwa kuhusishwa kikamilifu ambapo sisi tumejikita katika kulinda amani ya nchi,” alisema Nasir.

ZEC ipo katika harakati za maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba ikiwemo baadhi ya shughuli zilizofanywa ni kukamilisha kazi za uandikishaji wapiga kura katika daftari la kudumu na kulihakiki.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ecb4a04a96c9896a96af925cce88dfeb.jpg

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi