loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Katavi yauza madini ya bilioni 21.8/-

SERIKALI mkoani Katavi imeuza madini ya dhahabu yenye uzito wa kilogramu 233 yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 21.8 kwenye soko kuu la kununua madini tangu lilipoanzishwa rasmi Mei mwaka jana.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera akizungumza na wanahabari ofisi kwake mjini hapa, alisema tangu kuanzishwa kwa soko kuu la kununua madini Mei mwaka jana mkoani Katavi, mkoa huo umepiga hatua kubwa ya ongezeko la ununuzi wa madini ya dhahabu tofauti na ilivyokuwa awali.

Homera alisema Sh bilioni 21.8 zimetokana na ukusanyaji wa mrabaha, ada ya ukaguzi na tozo ya huduma za jamii katika halmashauri za mkoa huo.

“Tangu ununuzi wa madini ulipoanza Mei mwaka jana, dhahabu yenye uzito wa kilogramu 233 ikiwa na thamani ya shilingi 21,895,081.272 imeuzwa... Mei mwaka huu dhahabu yenye uzito wa kilogramu 30 ilinunuliwa ikilinganishwa na dhahabu yenye uzito wa gramu 139 iliyonunuliwa Mei mwaka jana.

“Ongezeko hili limesababishwa na wanyabiashara wote wenye leseni kununua madini hayo kwenye soko kuu la mkoa,” alisisitiza Homera.

Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu wa Mkoa wa Katavi, Willy Mbogo alisema idadi ya wachimbaji wa dhahabu wanaouza kwenye soko kuu imeongezeka kutokana na hamasa inayotolewa na uongozi wa chama hicho kwa kushirikiana na serikali.

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye, ametoa ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Mpanda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi