loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wajasiriamali Uganda wakimbilia Tanzania

MAKALI ya sheria ya kutotoka ndani ‘lockdown’ nchini Uganda, yamewalazimisha wajasiriamali wadogo wa nchi hiyo kuvuka mpaka na kuja kuendesha shughuli zao nchini Tanzania, wilayani Misenyi, mkoa wa Kagera.

Akizungumza na HabariLEO Afrika Mashariki jana, mmoja wa viongozi wa wafanyabiashara wilaya ya Misenyi, Hussein Muzo, alisema baada ya wafanyabiashara na wajasiriamali wa Uganda kubanwa na sheria ya ‘lockdown’ nchini kwao, waliamua kuja Tanzania kuendeleza biashara zao kwa ajili ya kujipatia fedha.

Alisema wajasiriamali hao wanachukua bidhaa mbalimbali ikiwamo nguo na viatu kutoka nchini Uganda na kuja kuuza nchini.

Alisema kutokana na hali hiyo, biashara katika wilaya ya Misenyi imechangamka kwa kupata wateja wengi kutokana na ongezeko la bidhaa za ndani ya Tanzania na kutoka Uganda.

Hata hivyo, Muzo alidai wafanyabiashara wa Tanzania wanojaribu ama kwa njia ya halali au njia za panya kuingiza bidhaa nchini Uganda, wanatandikwa viboko na maofisa usalama wa Uganda, lakini kwa upande wa Tanzania wanapokelewa na kufanyiwa vipimo vya corona kuona kama wapo salama na kuruhusiwa kuendelea na biashara zao.

“Tunashangaa kuona wafanyabiashara wa Uganda wanapimwa katika mpaka wa Mutukula na kuruhusiwa kuingia nchini na kufanya manunuzi na kupeleka kwao, lakini hakuna Mtanzania anayeruhusiwa kwenda kufanya biashara Uganda kwa kigezo cha corona,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, mkoani Kagera, Kanali Denice Mwila, amekiri kuwapo kwa wajasiriamali wa Uganda waliokuja nchini kufanya biashara ndogondogo hususani ya nguo na viatu.

Alisema serikali ya wilaya hiyo imejipanga kuwauzia vitambulisho vya wajasiriamali wafanyabiashara hao ili kuongeza makusanyo ya mapato katika muda ambao watakuwa wanafanya shughuli zao katika mkoa wa Kagera.

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye, ametoa ...

foto
Mwandishi: Selemani Nzaro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi