loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Lipumba- Wakati ukifika nitasema

CHAMA cha Wananchi (CUF) kinaendelea na vikao vya maandalizi ya ushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba huku Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba akisita kutamka kama atagombea urais au la.

Profesa Lipumba alisema uamuzi wa kugombea urais ni wa Mkutano Mkuu wa chama.

“Wakati ukifika mtajua kama Profesa atachukua au la,” alisema jana alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya uamuzi huo.

Alikuwa miongoni mwa viongozi wakuu wa vyama 19 vya siasa walioshiriki kikao cha Msajili wa Vyama vya Siasa, alisema chama kimeruhusu watu wanaendelea kuchukua fomu.

Akizungumza na gazeti hili, Naibu Katibu Mkuu Bara wa CUF, Magdalena Sakaya alisema upande wa Bara, yupo mmoja aliyemtaja kuwa ni Chief Liemba ambaye ameshachukua fomu ya kugombea.

Sakaya ambaye pia alikuwa kwenye kikao cha msajili wa vyama, alisema wako kwenye vikao vya kitaifa vya chama ambavyo pamoja na masuala mengine, wanajadili kuhusu wagombea.

Vikao hivyo ni pamoja na Kamati Tendaji, Kamati ya Uongozi, vikao vya Bodi ya Udhamini, kikao cha Baraza Kuu la Uongozi wa Taifa chenye uamuzi.

Alisema chama kimejiandaa vizuri kuweka wagombea kuanzia urais, wabunge na madiwani huku kikihamasisha wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali.

TRAFIKI Kanda Maalum Dar es Salaam imese- ma ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi