loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Klopp awatuliza mashabiki Liverpool

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amewataka mashabiki wa timu hiyo kusubiri hadi muda sahihi utakapowadia kusherehekea pamoja taji la kwanza la klabu hiyo la Ligi Kuu ya England baada ya miaka 30 kulisotea.

Maelfu ya mashabiki wa timu hiyo walishangilia jijini hapa Ijumaa, licha ya kuwapo katazo la mikusanyiko kwa sababu ya janga la virusi vya corona.

Watu wa Zimamoto walizima moto mdogo uliowashwa na mashabiki katika jengo la Liver na kusababisha watu 34 kuumia, huku watatu wakijeruhiwa. Klopp alisema hakufarahishwa na hali hiyo iliyotokea katikati ya mji wa Liverpool.

Katika barua yake ya wazi iliyochapishwa katika jarida la Echo mjini Liverpool, kocha huyo Mjerumani alisema: “Mimi ni binadamu na shauku yenu ndio shauku yangu, lakini kwa sasa kitu muhimu sana ni kwamba hatuna aina hii ya mikusanyiko.”

“Tafadhali, shangilieni, lakini kwa usalama na kwa faragha, huku mkijitahidi kuchukua tahadhari, kwani msichukulie poa ugonjwa huu ambao umesambaa sana katika jamii.”

Klabu hiyo ambayo imeshinda taji hilo kwa mara ya kwanza 30 iliyopita, ililalamika kuwa vitendo vilivyofanywa na baadhi ya mashabiki wake waliokusanyika vimesababisha Klabu ya soka ya Liverpool na jiji la Liverpool kudharaulika.

Watu pia walikusanyika nje ya Anfield Alhamisi baada ya Manchester City kufungwa na Chelsea 2-1 na kuihakikishia Liverpool kutofikiwa kwa pointi zozote na washindani wake wa karibu.

“Ikiwa mambo yalikuwa tofauti hakuna zaidi ya kushangilia pamoja, tutakuwa na gwaride ambalo litakuwa kubwa kuliko lile tulivyotwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka jana, hivyo tutashangilia pamoja.”

“Wote tulifanya mambo makubwa kupambana na covid-19 na juhudi hizi hatuwezi kuzipoteza hivi hivi tu. Wakati na muda utakapofika tutashangilia. Lakini kwa sasa, tafadhali bakini ikiwezekana nyumbani,” alisema Klopp.

MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich, Robert Lewandowski, amesema anadhani kocha wa ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi