loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RC Mwanri astaafu, JPM ateua wakuu wa mikoa 2 na ma-DC 9

Rais John Magufuli amemteua Dk Philemon Sengati kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuchukua nafasi ya Aggrey Mwanri ambaye amestaafu.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu na kusambazwa leo, Julai 3, 2020, inaeleza kuwa Rais amemteua aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma akichukua nafasi ya ya Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Mganga ambaye naye amestaafu.

Hata hivyo Rais John Magufuli amewateua wakuu wa wilaya tisa kujaza mapengo mbalimbali yanayotokana na kustaafu na kuhamishwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais ameteua aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido, mkoani Arusha, Toba Nguvila kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni kuchukua nafasi ya Godwin Gondwe ambaye anayehamia wilaya ya Temeke, mkoani Dar es Salaam kuchukua nafasi ya Felix Lyaniva ambaye amestaafu.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi