loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanandoa sasa ruksa kukodi farasi wa polisi

JESHI la Polisi kupitia Kikosi cha Farasi, limeanzisha huduma ya kukodisha farasi wake kwa ajili ya shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo sherehe ya harusi.

Hayo yamebainishwa na Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Dk Omary Lunyombe wakati akizungumza na gazeti hili jana katika Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam maarufu Sabasaba.

Alisema farasi hao wamebobea katika utoaji wa huduma mbalimbali katika jamii, kuanzia zinazohusiana na shughuli za kipolisi pamoja na masuala ya kijamii ikiwepo ubebaji wa raia.

Alisema kupitia uwezo wao huo, raia wanaweza kukodisha huduma hiyo. Aliwasihi wapendanao kutumia huduma ya farasi kwenye sherehe yao ya kufunga ndoa.

“Inafahamika kuwa wanandoa pindi wakiwa wanaenda kanisani au kutoka kanisani kwenda ukumbini wanatumia usafiri wa aina mbalimbali hususan magari, ni vema wakafahamu kuwa wanaweza hata kutumia huduma hii ya farasi inapatikana tena kwa bei nafuu,” alieleza Lunyombe.

Akizungumzia kuhusu farasi hao ambao pia ni askari, Lunyombe alibainisha kuwa farasi hao wana uwezo wa kufanya kazi za ulinzi, hasa kwenye maeneo yenye vurugu. Alisema Polisi imekuwa ikiwatumia farasi hao, kutuliza ghasia sehemu mbalimbali kwenye fujo, ikiwa ushiriki mzuri kwenye operesheni mbalimbali kubwa.

Gazeti hili likiwa kwenye hilo banda la Polisi, lilijionea farasi wawili na mbwa wawili wa jeshi hilo. Pia kulikuwa na boti kubwa ya kisasa, inayotumiwa na Jeshi la Polisi kufanya operesheni mbali mbali majini.

Aliwataka wananchi kufika kwenye banda hilo, ili kujifunza masuala kadhaa kuhusu utunzaji bora wa mbwa pamoja na namna mbwa anavyoweza kutumika kama askari majumbani.

MGOMBEA Urais kwa tiketi ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

1 Comments

  • avatar
    Shadrack
    09/08/2020

    Habari, naomba kujua gharama zakukodi farasi wawili nipo moshi mjini

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi