loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Harmonize aishauri Basata ianzishe tuzo

STAA wa Bongo Fleva, Rajab Kahali au Harmonize, ametoa ushauri kwa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kuanzisha tuzo za muziki nchini, ili kuwatangaza wasanii wenye kazi bora.

Msanii huyo alitoa ushauri huo juzi Dar es Salaam, ambapo alisema Basata kama mlezi wa masuala ya sanaa, hawajaanzisha tuzo zozote za kutambua mchango wa wanamuziki wenye kazi bora licha ya kutoa mchango kwenye kushughulikia maudhui ya kazi zao.

Harmonize ambaye ni Rais wa Lebo ya Kondeboy, alisema wasanii wengi wamebaki kushindana kwenye mitandao ya yotube, kwa kuangalia msanii ambaye nyimbo yake imetazamwa na watu wengi.

“Bila tuzo Tanzania ni sawa na kujitekenya na kucheka mwenyewe na kutumia nguvu kuwaaminisha watu kuwa wewe ni bora au muziki wako ni bora zaidi, ni ngumu kujua kazi zako zina mapokezi gani maana wanaojirekodi video na kukutumia ni mashabiki zako, wale ambao sio mashabiki zako mtazamo wao huujui,” alisema Harmonieze.

Aliitaka Basata kuangalia suala hilo na kuona umuhimu wa kuanzisha tuzo ili kuwasaidia wasanii wanaofanya vizuri na sio kuacha mfumo wa watu kutumia nguvu kwenye mitandao kwani haiwezi kusaidia kukuza muziki wa Tanzania.

“Tuzo ni kipimo kizuri cha msanii yeyote duniani kujua wapi amelegeza ili akaze akikosea, zinakufanya ujitambue na ujue thamani yako, pia zinatia moyo na hamasa ya kufanya kazi, siongeagi sana ila inahuzunisha, tunahitaji kuwa na tuzo za muziki Tanzania, zisimamiwe na Basata wenyewe,” alisema.

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 4 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 4 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 5 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...