loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Takukuru kuhoji wasimamizi wa mgodi

MKURUGENZI wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), John Mbungo ameagiza kuitwa mara moja wasimamizi wa mgodi wa North Mara kuhojiwa na taasisi hiyo mkoani Mara kutokana na madai ya kuchelewesha malipo ya wafanyakazi wa kampuni hiyo walioumia kazini.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya wawakilishi wa waliokuwa wafanyakazi hao wanaokadiriwa kuwa 44 ambao wanadai kupata ulemavu wa kudumu wakiwa kazini mgodini hapo kufika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Takukuru mjini Dodoma wakilalamikia kupunjwa malipo yao.

Mbungo aliliambia HabariLEO kwa njia ya simu kwamba wasimamizi wa mgodi huo wanapaswa kujieleza kwa nini wameshindwa kutekeleza malipo halali ya waliokuwa wafanyakazi kwa mujibu wa mikataba yao na kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 10.

“Nilipokea malalamiko kutoka kwa waliokuwa wafanyakazi wa kampuni hiyo iliyopo wilayani Tarime kuhusu kupunjwa malipo yao halali na taasisi yetu (Takukuru) imelazimika kumwita meneja wa mgodi huo ajieleze kwanza kwa nini suala la fidia ya kuumia kazini limechukua muda mrefu kutatuliwa,” alisema.

Mkurugenzi alisema taasisi hiyo ilianzisha uchunguzi kuhusu matukio ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka kuhusiana na malipo ya fidia mbalimbali zinazotekelezwa na mgodi huo kwa wananchi ambao pia wanatuhumiwa kuvamia maeneo yaliyofanyiwa tathmini na kujenga majengo upya kwa ajili ya kudai malipo ya ‘Tegesha’.

Katika hatua nyingine aliwataka viongozi wa serikali waliopo ngazi za mkoa na wilaya kutimiza wajibu wao wa kuhudumia wananchi kwa kutatua kero zao kwa wakati kwenye maeneo yao kote nchini, wakitanguliza uzalendo ambapo wananchi wanalazimika kukimbilia ofisi za kitaifa.

“Matukio ya hivi karibuni kwa wananchi kuamua kukimbilia ofisi kuu za kitaifa na kusubiri kujieleza mbele ya ziara za viongozi wa kitaifa ili kutafuta ufumbuzi wa kero zao ni ishara kwamba huenda ngazi za chini za utawala zinashindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo,”alisema.

JUMLA ya Dola za Marekani milioni 779 zimepatikana kutokana na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi