loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dawa ya corona ya NIMR yawa dili EAC

WAFANYABIASHARA nchini wamechangamkia biashara ya dawa iliyotengenezwa na Taasisi ya Utafi ti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu (covid-19), kwa kuipeleka kuuza katika nchi za Afrika Mashariki zinazokabiliwa na ugonjwa huo.

Dawa hiyo iliyopewa jina la NIMRCAF, inatokana na mchanganyiko wa vyakula na mitishamba na katika majaribio imeonesha ina uwezo mkubwa wa kudhibiti virusi vya corona vinavyosababisha ugojwa huo.

Licha ya kuwa hakuna serikali ya nchi za EAC iliyotoa ombi la kutaka kupatiwa dawa hiyo, lakini imesambaa katika baadhi ya nchi za EAC ambako imepelekwa na wafanyabiashara hao.

Mbali na kuonekana nchini Kenya, dawa hiyo pia imeonekana ikiuzwa katika nchi za Rwanda na Uganda. Mkurugenzi wa Kitengo cha Tiba Asili cha NIMR, Dk Justine Omolo, akizungumza HabariLEO jana, alisema wana taarifa ya kuonekana dawa hiyo katika nchi zinazopakana na Tanzania na kwinginezo.

“Hakuna ombi maalum tulilopata kutoka nchi za EAC kuhitaji dawa hii ili kusaidia kupambana na ugonjwa huo, lakini inaonekana wafanyabiashara wamechangamkia fursa kwani zinaonekana huko zikiuzwa kwa kasi,” alisema.

Alisema awali walianza uzalishaji wa chupa 800 kwa siku, lakini sasa wanazalisha chupa 8,000 kwa siku na wakati maambukizi ya homa hiyo yalipokuwa yapo juu nchini, walikuwa wakiuza kwa kiasi kikubwa tofauti na sasa.

Alisema kwa sasa chupa 2,000 zinachukuliwa kwa siku na watu wengi wamekuwa wakitumia kama kinga, ikiwamo kuwapatia wanafunzi waliopo shule za bweni. Dk Omolo alisema wafanyabiashara wanaoenda kuchukua dawa hiyo hawaulizwi wanaenda kuuza wapi, lakini zimeonekana zikivushwa mipakani.

Alisema ili kuhakikisha dawa hiyo inapelekwa kwenye nchi za EAC, wanategemea Jumuiya ya Afrika Mashariki ingefanya ushawishi na balozi za nchi husika zingetumika kuzungumza na NIMR ili iweze kufikishwa katika nchi hizo.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi