loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watia nia CCM, ACT na NCCR kuanikwa kesho

VYAMA vya siasa nchini vimesema vitatangaza majina ya walioomba kuwania nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani kuanzia kesho hadi Julai 17 mwaka huu.

Viongozi wa vyama vya siasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ACT- Walendo na NCCR-Mageuzi, walisema majina hayo na idadi ya wagombea yatatangazwa kuanzia siku hiyo hadi Julai 17 mwaka huu, kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza na HabariLEO, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema utaratibu wa watia nia na wachukuaji fomu za kugombania ubunge, uwakilishi na udiwani katika chama hicho watajulikana kesho, lakini kwa sasa hawezi kuzungumzia suala hilo.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo, Ado Shaibu, alisema utoaji fomu katika majimbo na kata zote umeanza tangu Julai mosi hadi 13 mwaka huu, ambayo ndio siku ya mwisho kuchukua na kurejesha fomu.

Alisema utoaji fomu unaendelea vizuri licha ya kusema hana idadi hadi sasa waliochukuwa kwa vile makatibu wa matawi kichama bado hawajawasilisha orodha ya watu waliochukuwa fomu lakini alisisitiza kuwa wanachama ni wengi waliojitokeza kugombea nafasi za uongozi katika chama hicho.

Alieleza wapo waliofika katika jimbo moja watu 30 waliochukuwa fomu za ubunge na nafasi nyingine lakini takwimu hizo zitatolewa Julai 13 ambapo ndio siku ya mwisho kurejesha na kuchukua fomu.

Alisisitiza sio vyema kutoa takwimu kwa sasa kwa vile wapo wengine huwa wanachukuwa, lakini pia wanashindwa kurejesha fomu kwa sababu moja ama nyingine.

Aidha alifafanua kuwa hadi sasa hana idadi kamili ya wanachama waliochukuwa na kurejesha fomu, ambapo takwimu kamili ataweza kuitoa Julai 13, baada kazi hiyo kukamilika. Mapema Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi (CCM), Humphrey Polepole, alisema kumejitokeza muitiko mkubwa katika Chama cha Mapinduzi, kwa vile kila mwanachama anajitambua anakwenda kutia nia ya kugombea nafasi ya ubunge, uwakilishi na udiwani, katika hatua ya awali.

Alisema CCM ni chama kinachoangaliwa na watu wengi kwamba kina uwezo mkubwa wa kutoa viongozi bora watakaoongoza nchi kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, hivyo utoaji wa fomu rasmi utaanza Julai 14 hadi Julai 17 mwaka huu, ambapo baada ya hapo wataweza kutoa idadi halisi ya wagombea katika majimbo na kata zote za Tanzania.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: Mwanajuma Abdi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi