loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kwanza TV ya Maria Sarungi yafungiwa tena

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeifungia Kwanza Online Tv inayomilikiwa na Maria Sarungi kutotoa huduma za utangazaji kwa kipindi cha miezi 11 baada ya kuchapisha taarifa ya upotoshaji inayodaiwa kutolewa na Ubalozi wa Marekani nchini.

Hatua hiyo, imekuja siku chache baada ya kumaliza kifungo cha miezi sita walichoanza Septemba 28, mwaka jana kutokana na kuchapisha habari isiyo na ukamilifu na kutoweka sera na mwongozo wa watumiaji kwenye mtandao wao.

Akitoa taarifa hiyo jana jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui, Joseph Mapunda alisema Julai Mosi mwaka huu kituo cha Kwanza Online Tv kupitia ukurasa wake wa Instagram ilikiuka kanuni za utangazaji kwa kuchapisha taarifa inayodaiwa kutolewa na ubalozi huo.

Alisema taarifa hiyo ilijaa upotoshaji kwa jamii bila kufuata usahihi na ukweli wa taarifa husika, na bila kuzingatia mizania ya habari. Alisema katika utetezi wa kimaandishi uliowasilishwa mbele ya Kamati hiyo, uongozi wa Kwanza Online Tv ulidai kuwa unapinga mashtaka husika kwani imetoa taarifa inayotumika matakwa ya Katiba chini ya Ibada ya 18, inayompa mtu uhuru wa kutoa maoni yoyote, mawazo, kutafuta na kutoa habari kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi.

Mapunda alisema uongozi huo uliiambia kamati kuwa walichapisha habari hiyo kwa lengo la kuhakikishia umma juu ya maoni ya ubalozi huo kuhusu virusi vya corona.

“Walidai kuwa asili ya habari hiyo ni kwamba haikuwa na mantiki wala haja ya kutafuta upande wa pili kwani taarifa hiyo ilikuwa ni taarifa kwa umma na sio aina ya taarifa ambayo inahitaji upande wa pili kwani ulikuwa ni msimamo na maoni ya ubalozi,” alieleza Mapunda.

Alisisitiza kuwa kituo hicho kilidai uzalendo wao ulikuwa ni kujulisha umma kuwa mataifa mengine yanazungumzia nini kuhusu Tanzania na ni hatua gani nchi inatakiwa kuchukua ili kuepuka minong’ono kutoka mataifa mengine.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi