loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Muhimbili yahudumia wagonjwa 385 Sabasaba

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili imehudumia wagonjwa 385 katika banda lake lililopo kwenye Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu Sabasaba ambapo kati yao wapo waliopatiwa tiba ya uchunguzi wa macho, saratani ya matiti na huduma za dharura.

Akizungumzia huduma katika banda hilo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha alibainisha kuwa kwa muda wa siku tano tangu kuanza kwa maonesho hayo, idadi hiyo ya wananchi waliojitokeza inatia matumaini.

Alisema inaonesha ni kwa kiasi gani kuna uhitaji wa huduma za macho, saratani ya matiti kwa wananchi na ndio maana kwa kutambua hilo Muhimbili ikaamua kuwasogezea huduma kwa ukaribu zaidi.

Alisema kati ya wananchi hao, 214 wameonwa kwenye kliniki ya macho, 56 kliniki ya saratani ya matiti na 115 kupitia idara ya magonjwa ya dharura. Pia wananchi 30 wamepewa rufaa ya matibabu zaidi katika Hospitali za Muhimbili zilizopo Upanga na Mloganzila.

“Wananchi 51 wamepata miwani ya kusomea ambayo inapatikana hapahapa katika banda letu la Sabasaba kuchangia gharama kidogo ya Sh 10,000,”alisema.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi