loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

AFD kuipatia Rwanda euro milioni 49.5

BENKI ya Maendeleo Ufaransa (AFD) imesaini makubaliano na serikali ya Rwanda katika maeneo mawili yenye thamani ya Euro milioni 49.5 (faranga bilioni 54), ikiwamo kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

Makubaliano hayo yalisainiwa na Waziri wa Fedha na Uchumi wa Rwanda, Uzziel Ndagijimana na Ofisa anayeshughulikia masuala ya mambo ya ndani wa Ufaransa nchini Rwanda, Jeremie Blin, ikiwa ni sehemu ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Ndagijimana alisema eneo la kwanza linahusu euro milioni 40, ikiwa ni mkopo wa bajeti (takribani faranga bilioni 42.5) kwa ajili ya kuweka mikakati ya kukabili kuenea kwa virusi vya corona, pamoja na mipango ya kurejesha uchumi.

Katika usalama kwa jamii, Blin alisema huduma zitawafikia wananchi 620,000 walioathirika na ugonjwa wa covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona kwa kuwapatia fedha taslimu au kazi kwa kaya zenye uhitaji, pamoja na programu za lishe kwa wajawazito na kutoa bima kwa watu zaidi ya milioni 1.9. Waziri huyo alisema mkopo huo utalipwa kwa miaka 26 bila kuwa na riba.

Nyongeza ya mkopo wa bajeti ya euro milioni 40, AFD imeahidi kutoa msaada wa euro milioni mbili (takribani faranga bilioni 2.1) kwa shirika la msaada la Msalaba Mwekundu kwa ajili ya kuzisaidia kaya zilizokabiliwa na ugonjwa huo.

Ndagijimana alisema mkataba wa pili wa euro milioni 5.8 (takribani faranga bilioni sita), utasaidia nchi kuendeleza mfumo wa mafunzo ya ufundi ili kuongeza ajira kwa vijana kupitia vyuo vya mafunzo ya ufundi.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi