loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Kagame atoa baiskeli 589 kwa viongozi wa vijiji

RAIS Paul Kagame (pichani) ametoa baiskeli 589 kwa viongozi wa vijiji 18 vinavyozunguka msitu wa Nyungwe, kwa ajili ya kuwashukuru kwa kazi za kuhudumia jamii.

Rais Kagame ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rwanda, aliwapa zawadi hiyo viongozi hao kutokana na kufanya kazi kubwa kukabiliana na makundi ya watu wenye silaha waliovamia maeneo hayo na kujaribu kudhoofisha nchi hiyo.

Makundi hayo kutoka nchi jirani yanadaiwa kuvuka mipaka mara kwa mara kwa kutumia msitu huo na kujaribu kuvamia na kuua watu wasio na hatia na kuharibu mali zao.

Hata hivyo,vikundi vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na viongozi wa maeneo hayo na wananchi wamekabiliana nao vikali na kudhibiti uvamizi huo. Baiskeli hizo zilikabidhiwa kwa viongozi wa vijiji vya wilaya za Nyaruguru, Karongi, Nyamasheke na Rusizi.

Rais Kagame alisema ushirikiano kati ya taasisi za ulinzi, viongozi wa vijiji na wananchi kwa ujumla, umethibitisha kuwa wananchi wa nchi hiyo ni wamoja na wako tayari kupambana na adui yeyote atakayejaribu kudhoofisha nchi.

Kiongozi wa kijiji cha Nyacyondo, Emmanuel Nubahimana, alisema zawadi hizo ni hamasa kwao kuendelea kushirikiana na taasisi za ulinzi katika ulinzi wa nchi.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi