loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mkandarasi maegesho ya ndege Uwanja wa Karume abanwa

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imeitaka kampuni kutoka China ya BCG, inayojenga maegesho ya ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, kukamilisha mradi huo ifi kapo Septemba mwaka huu na kuukabidhi serikalini.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mohamed Ahmada, alisema hayo alipotembelea mradi huo kuona maendeleo yake jana. Mradi huo unagharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Alisema wizara inataka kuona mradi huo wa maegesho ya ndege, unakamilika kabla ya kumalizika kwa Awamu hii ya Rais Ali Mohamed Shein.

‘’Serikali inataka kuona kwamba mradi huu unakamilika ifikapo mwezi wa Septemba kabla ya kumalizika kwa kipindi cha urais wa Dk Shein ambaye amekuwa akifuatilia kwa karibu sana,’’ alisema.

Ahmada alisema mradi wa jengo la abiria la Uwanja wa Ndege wa Zanzibar na maegesho ya ndege, ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati, yenye lengo la kuongeza mapato kwa taifa.

Alisema miradi hiyo itakapomalizika, itaongeza kwa kiwango kikubwa watalii hadi kufikia 600,000 kutoka 540,000 mwaka 2018/2019. Awali, Mkandarasi wa mradi huo, Yassir De Costa, aliahidi kuukamilisha kwa wakati, lakini kwamba anahitaji nguvu kazi zaidi ya wafanyakazi.

‘’Tunaendelea na kasi ya kumaliza mradi wa maeneo ya maegesho ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa wakati ifikapo Septemba...tunahitaji nguvu kazi ya wafanyakazi ili kufikia tamati ya mradi huu,’’ alisema.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi