loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mfumuko wa bei watulia

MFUMUKO wa bei wa taifa umebaki ule ule kwa mwaka unaoishia Juni 2020 wa asilimia 3.2 kama ulivyokuwa kwa mwaka unaoishia Mei, mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini hapa jana, Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), Ruth Minja alisema mfumuko huo unaopima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi haujabadilika katika kipindi hicho.

Minja alisema kutobadilika huko, inamaanisha kwamba kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka unaoishia Juni 2020 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka unaoishia Mei, mwaka huu.

Ruth alisema mfumuko wa bei wa mwaka unaoishia Juni mwaka huu haujabadilika, lakini umechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa bei za baadhi za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula katika kipindi hicho kinachoishia Juni, mwaka huu zikilinganishwa na bei za Juni mwaka jana.

Alisema baadhi ya bidhaa za vyakula zilizopungua bei kwa Juni, mwaka huu zikilinganishwa na bei za Juni mwaka jana, ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia 1.6 na matunda kwa asilimia 2.1. Bidhaa nyingine ni viazi mviringo kwa asilimia tano na mihogo kwa asilimia 13.3.

Kwa upande mwingine, baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoongezeka bei kwa Juni, mwaka huu ukilinganisha na bei za Juni mwaka jana, ni pamoja na mavazi kwa asilimia 2.7.

“Nyingine ni gesi ya kupikia kwa asilimia 7.8, mkaa kwa asilimia 11.2, samani kwa asilimia 2.7 na vitabu vya shule kwa asilimia 1.5,” alisema.

Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka unaoishia Juni mwaka huu umepungua hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 4.4 kwa mwaka unaoishia Mei 2020.

Hali ya mfumuko katika Afrika Mashariki (EAC) kwa mwaka unaoishia Juni, mwaka huu, nchini Kenya inaonesha kwamba umepungua hadi asilimia 4.59 kutoka asilimia 5.33 kwa mwaka unaoishia Mei, mwaka huu.

JUMLA ya Dola za Marekani milioni 779 zimepatikana kutokana na ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi