loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Vodacom yaipongeza Simba

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom, ambayo ndiyo mdhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara, imeipongeza Simba kwa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 20. Simba ndiye bingwa wa msimu wa mwaka 2019/2020 na jana ilikabidhiwa rasmi taji jilo.

Pia kampuni hiyo imezipongeza timu zote zilizoshiriki VPL msimu huu.

Pongezi hizo zilitolewa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom, Linda Riwa ambaye alisema:

"Tunajivunia sana kuwa sehemu ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwani inaendelea kukua na kuboreshwa mwaka hadi mwaka.

“Pongezi zetu pia ziwaendee viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi, klabu zote zilizoshiriki, waandishi wa habari na wengine wote“.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 3 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 3 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 3 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...