loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watanzania tumieni miundombinu inayojengwa kuwekeza

SERIKALI ya Rais John Magufuli tangu ilipoingia madarakani mwaka 2015, imekuwa mstari wa mbele kuimarisha miundombinu ya barabara, reli, maji na sekta ya anga.

Serikali imekuwa ikifanya hivyo ikiamini kuwa ukarabati wa miundombinu hiyo, ndiyo chachu ya kukuza uchumi wa taifa letu. Kwa mfano, ujenzi wa reli umeifanya Tanzania kupanda na kuwa mojawapo wa nchi za kipekee za Afrika, ambazo zina miundombinu bora ya reli.

Mpaka sasa Tanzania inategemea kuanza kusafirisha abiria kwa kutumia treni za mwendokasi, zitakazotumia nishati ya umeme.

Miundombinu ya barabara nayo imeimarishwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari, ambao ni tatizo sugu katika maeneo mengi.

Ukarabati huo umehusisha ujengaji wa barabara za juu na uanzishwaji wa mabasi yaendayo kasi, ambayo yamekuwa ni mwarobaini wa kutibu matatizo yote hayo. Juhudi hizo ambazo serikali inazifanya ili kukuza nchi kiuchumi, zimefungua fursa nyingi za ajira na kuwezesha wananchi kujikwamua kiuchumi na taifa kupiga hatua za maendeleo.

Hivyo, kimsingi Watanzania wanapaswa kutumia kikamilifu fursa hizo, badala ya kukaa mitaani na kuilaumu serikali juu ya ukosefu wa ajira wakati ajira zingine tumeziacha zikachukuliwa na wageni, ambao siyo wazawa wa taifa hili.

Tunapaswa tuitumie miundombinu hiyo kama chachu ya maendeleo yetu binafsi, kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali, kama kilimo, biashara na elimu, ili ziendane na Tanzania ya sasa, ambayo inakua kwa kasi.

Jambo hili lisiishie tu kwa mwananchi wa kawaida tu, bali lihusishe pia wafanyabiashara wakubwa waliopo nchini, ili kupanua wigo mkubwa zaidi wa kibiashara kwa kufikisha huduma zao kote nchini.

Aidha, inatakiwa kuacha kuitazama Dar es Salaam, kama ndiyo mji pekee wa kibiashara, bali inatakiwa kutazama pia na miji mingine.

Kwa upande wa sekta ya elimu, wanafunzi na wadau wote wa elimu waangalie suala hili, kwa kuandaa wasomi ambao wataendana na fursa hizi ambazo zinaendelea kukua katika nchi yetu, kwa kuandaa mafundi na madereva wa vyombo ambavyo vinaendelea kuletwa nchini.

Miundombinu hii imejengwa kwa ajili yetu sisi na inabidi itunufaishe sisi wenyewe wazawa kwa kutuongezea kipato, tofauti na hapo mwanzoni ambapo kulikuwa na miundombinu mibovu na isiyo rafiki uchumi wa nchi kukua. Naipongeza serikali kwa juhudi inazoendelea kufanya katika kukuza uchumi, hali iliyowezesha nchi kupanda na kuwa moja ya nchi zenye uchumi wa kati.

WAKATI zikiwa zimebaki siku ...

foto
Mwandishi: Mwanahija Said, Udom

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi