loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Nchi ina petroli ya kutosha’

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema nchi ina kiasi cha kutosha cha bidhaa za mafuta ya petroli na kwamba mfumo wa uagizaji mafuta kwa pamoja umesaidia kuondoa kero ya bidhaa hizo kuadimika sokoni.

Hayo yalibainishwa na Meneja Mawasiliano wa Ewura, Titus Kaguo kwenye banda ya mamlaka hiyo katika Viwanja vya Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya biashara ya Dar es Saalam (DITF), yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba jijini humo.

Kaguo alisema kwa mujibu wa ripoti ya mpya ya mwaka 2018/19 ya Ewura, iliyotolewa hivi karibuni, nchi ina mafuta ya kutosha ya petroli na hadi sasa hakuna ukosefu wa bidhaa hiyo sokoni.

Aidha alisema katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 2019, jumla ya lita za nishati ya petroli 5,753,118,081 ziliingia nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam,Tanga na Mtwara.

Hata hivyo, kiwango hicho alikitaja kupungua kwa asilimia nne ukilinganisha na mwaka uliotangulia wa 2017/2018 ambapo lita za petroli na nishati nyingine zilizoingia zilikuwa 5,993,954,008.

“Utaona pamoja na kiasi cha nishati ya petroli na bidhaa zake kupungua kwa asilimia nne ukilinganisha na mwaka uliopita, bado nchi haina uhaba wa nishati, tumehakikisha upatikanaji na bidhaa hiyo nchi nzima unakuwepo, uagizaji wa mafuta wa pamoja umesaidia kuondoka uhaba na sisi tunasimamia vizuri wajibu wetu ili mahitaji ya nishati hii muhimu isipungue na kuathiri soko,” alisema Kaguo.

Akizungumzia kiasi cha mafuta hayo kilichouzwa kwenye soko la ndani, Kaguo alisema kati ya lita 5,753,118,081 zilizoingia kupitia bandari hizo, lita 3,280,315,105 ziliuzwa nchini ikiwa ni sawa na asilimia 57 ya nishati yote ya petroli iliyoingia nchini kupitia bandari tajwa.

Aidha lita 2,472,802,976 za nishati za petroli kati ya lita 5,753,118,081 zilizoingia nchini zilisafirishwa kwenda nchi jirani ambayo ni sawa na asilimia 43 ya bidhaa hiyo yote.

Akuzungumzia bei za petroli sokoni Kaguo alisema EWURA inaendelea kusimamia na kupanga bei ya soko kulingana na bei ya dunia na kwamba wafanyabiashara wote wa bidhaa hizo wanafuata sheria na bei elekezi ili kusiwepo na kupandisha bei isivyo halali.

Mbali na bidhaa za petroli zilizoingia nchini katika ripoti hiyo ya EWURA pia imeonesha kiwango cha nishati ya gesi ya iliyosindikwa (LPG) kilichoingia nchini na kutumika kwenye matumizi mbalimbali ikiwemo kupikia kilichoingia nchini.

Ripoti hiyo inaonesha kuwa jumla ya metriki tani 145,800 za gesi ziliingia nchini katika mwaka wa 2018/19 ukilinganisha na metriki tani 120,961 kilichoingia mwaka uliotangulia.

JUMLA ya Dola za Marekani milioni 779 zimepatikana kutokana na ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi