loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maadhimisho ya Nanenane kitaifa kufanyika tena Simiyu

MAADHIMISHO ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yanafanyika kitaifa mkoani Simiyu kwa mara ya tatu mfululizo yakiongozwa na kauli mbiu inayohamasisha kuchagua viongozi bora watakaokuwa chachu ya mapinduzi kwa ajili ya kuinua ustawi wa wakulima, wafugaji na wavuvi.

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema maadhimisho hayo yataanza Agosti Mosi hadi Agosti 8 katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi, Simiyu. Kwa mara ya kwanza, maonesho hayo yalifanyika mwaka 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Songwe, Hasunga alisema kaulimbiu ya maonesho ni ‘Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020’.

Alisema kaulimbiu hiyo inatoa hamasa kwa wananchi kuchagua viongozi bora watakaokuwa chachu ya kuleta mapinduzi kwa ajili ya maendeleo ya sekta za kilimo kuinua ustawi wa maisha ya wakulima, wafugaji na wavuvi.

Waziri alisema maonesho yataambatana na uhamasishaji wa matumizi ya teknolojia bora za kilimo, ufugaji na uvuvi. Pia yatashirikisha wadau mbalimbali zikiwemo wizara, taasisi za mmma na binafsi, wabia wa maendeleo, wakulima na vyama vya wakulima, wafugaji na wavuvi.

Maonesho hayo ya 28 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993 yatafanyika kwenye Kanda nane za maonesho ambazo ni Kanda ya Mashariki (Morogoro), Kaskazini (Arusha), Magharibi (Tabora), Kusini (Lindi), Kati (Dodoma), Nyanda za Juu Kusini (Mbeya), Ziwa Mashariki (Simiyu) na Kanda ya Ziwa Magharibi (Mwanza).

Viongozi mbalimbali wa kitaifa watatembelea viwanja vya maonesho na kuhamasisha masuala mbalimbali ya kuendeleza sekta za kilimo, mifugo, uvuvi pamoja na Ushirika. Waziri ameagiza wadau wote wa sekta ya umma na binafsi kukamilisha maandalizi ya kushiriki katika viwanja vyote vya maonesho vilivyopo kwenye kanda.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi