loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kifaa cha kupima hali ya hewa chahakikiwa

KIFAA kilichobuniwa kukusanya takwimu za hali ya hewa kiko katika majaribio kupimwa ili kuangalia ubora na uhakika wa takwimu zake. Hayo yamesemwa na Meneja Mradi wa Utafiti Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Daud Mboma jijini Dar es Salaam juzi.

Alisema kifaa hicho kitakusanya takwimu za joto la hewa, kasi ya upepo, uelekeo wa upepo, mionzi ya jua pamoja na unyevu wa udongo. Alisema mradi huo umetengeneza kanzidata za kuhifadhi taarifa za kifaa hicho kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

“Mradi umeweza kuboresha mfumo wa usambazaji wa taarifa ya hali ya hewa kwa wakulima nchini za hali ya mvua katika msimu, hali ya mvua katika siku 14, na wakulima wamenufaika kwa kutumwa ushauri wa namna bora ya kulima kilimo chenye tija kulingana na hali ya hewa ya kipindi hicho,” alisema.

Mboma alisema kuna wakulima 20,000 waliopo katika mfumo na walikuwa wakitumiwa taarifa hizo na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini. Alisema mradi huo ulioanza mwaka 2013 utamalizika mwaka huu ukiwa umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Norway (Norad) na ukishirikisha wadau Chuo Kikuu cha Makerere Uganda, Chuo Kikuu cha Juba Sudan Kusini, Chuo Kikuu cha Bergen Norway na DIT.

Mradi huo umejikita kwenye maeneo makuu manne ya mfumo wa ukusanyaji wa taarifa za hali ya hewa, mfumo wa utunzaji wa taarifa za hali ya hewa, mfumo wa usambazaji wa hali ya hewa na mifumo ya uchakataji wa taarifa. Alisema katika maeneo yote hayo, mradi umelenga kuboresha tafiti na mafunzo.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi