loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Atozwa faini 500,000/- kwa kukutwa na kobe

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imemhukumu mfanyabiashara, Daniel Chizua kulipa faini ya Sh 500,000 au kwenda jela miaka miwili baada ya kukiri kukutwa na kobe wawili bila kibali halali.

Pia mshitakiwa huyo alitakiwa kulipa fidia ya Sh 650,000 baada ya kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) fedha ambazo tayari zimeingizwa akaunti ya serikali.

Akitoa adhabu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashidi Chaungu alisema mahakama inamtia hatiani mshitakiwa kwa kukiri kosa mwenyewe na kuingia makubaliano. Kabla ya kupewa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Ladislaus Komanya alidai hawana kumbukumbu ya makosa ya nyuma ya mshitakiwa lakini akaomba atekeleze makubaliano aliyoingia na DPP na kuiomba mahakama itoe adhabu kwa taratibu za kisheria.

Chizua aliiomba mahakama isimpe adhabu kali akidai amejifunza kutokana na makosa, atakuwa balozi ili watu wengine wasitende makosa hayo.

“Naomba mahakama inipe adhabu ndogo kwa sababu nina familia inayonitegemea ikiwemo mke, mtoto na wazazi,” Chizua alijitetea.

Chizua anadaiwa Januari 22, mwaka huu huko Masaki, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, alijihusisha na nyara za serikali kwa kukutwa na Kobe wawili hai wenye thamani ya Dola 140 sawa na Sh 320,600 mali ya Jamhuri ya Muungano bila leseni ya kuwa na nyara hizo kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi