loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RC aonya viongozi maeneo inakolimwa bangi

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Idd Kimanta amewataka viongozi wa vijiji na kata sehemu inakolimwa dawa za kulevya aina ya bangi Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, kudhibiti kilimo hicho vinginevyo watawajibishwa.

Kimanta alisema hayo juzi katika mkutano na watendaji wa vijiji 96 vya Wilaya ya Arumeru na kata 54 za Majimbo ya Arusha na Meru na watendaji wote wa Halmashauri ya Meru na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kujitambulisha na kupanga mpango kazi ikiwemo udhibiti wa bangi Arumeru.

Alisema anasikitishwa kuona bangi inalimwa miezi mitatu na wa nne inavunwa wakati Mtendaji wa Kijiji, Kata na Tarafa wapo na hakuna hatua zinachukuliwa dhidi ya wakulima na wahalifu hao.

Alisema hilo halitawezekana kwani kila mmoja anapaswa kuwajibika kwake. Mkuu huyo alisema kuanzia sasa Mtendaji wa Kijiji na Kata ya Mwandet eneo ambako bangi imelimwa na kuhifadhiwa vijiji vya Monduli, wanapaswa kusimamishwa kazi na Katibu Tarafa naye achunguzwe ndani ya siku 14.

Alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, kukaa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo kuongeza uwajibikaji kudhibiti bangi kwani tatizo hilo ni sugu wilayani humo.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi