loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

ZEC yaweka wazi majina ya wapiga kura

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imeanza kubandika majina ya wapiga kura katika vituo vya kupigia kura, ambapo wananchi wanatakiwa kwenda kuhakiki majina yao, ikiwa ni hatua ya kuelekea uchaguzi mkuu.

Mkurugenzi wa tume hiyo, Thabit Idarous Faina, alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa. Alisema ubandikaji majina ya waliojiandikisha katika vituo vya kupiga kura ni kwa mujibu wa Sheria ya uchaguzi Zanzibar namba 4 ya mwaka 2018, kifungu cha 19 (1), baada ya kumalizika kwa uandikishaji wapiga kura. Alisema lengo la kubandika majina hayo ni kutoa fursa kwa wapiga kura kuhakiki majina yao kuona kama yameandikwa kwa usahihi.

“Katika majina hayo, mtu pia anaruhusiwa kuweka pingamizi juu ya mtu aliyekosa sifa ambaye yumo katika orodha ya wapiga kura katika kituo hicho.”

‘’Kwa muda wa wiki moja, wapiga kura waliosajiliwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatakiwa kuhakiki majina yao ambayo yatabandikwa katika vituo vya kupiga kura katika majimbo yao. Zoezi hili ni muhimu kwani lengo lake ni kuondoa kasoro na malalamiko yanayoweza kujitokeza wakati wa upigaji kura katika vituo,’’ alisema.

Aidha, Faina alisema ZEC imejipanga kuhakikisha uchaguzi mkuu utakuwa huru na kasoro zote zinazoweza kujitokeza mapema zitapatiwa ufumbuzi wa haraka.

‘’ZEC tumejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi mkuu unakuwa huru na haki na ndiyo maana tumeanza utaratibu wa kuweka hadharani orodha ya wapiga kura wote kwa ajili ya kuhakiki majina yao,’’ alisema.

Makamu Mwenyekiti wa ZEC, Mabrouk Jabu, aliwataka wananchi waliojiandikisha kwenda katika vituo vya kupigia kura kuhakiki majina yao.

‘’Utaratibu wa kuweka majina ya wapiga kura hadharani ni muhimu, kwa sababu unawahakikishia wapiga kura nafasi ya kushiriki katika uchaguzi mkuu na kuzitambuwa mapema kasoro zinazoweza kujitokeza,’’ alisema.

ZEC ipo katika matayarisho ya mwisho ya kuelekea uchaguzi mkuu baada ya kuandikisha wapiga kura, pamoja na kuhakiki majina na kufuta wapiga kura waliopoteza sifa ikiwemo waliofariki dunia.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi