loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jafo aagiza meneja Tarura jiji la Arusha kuhamishwa

WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, ameagiza Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura) jiji la Arusha, Fordia Mwankenja, kuhamishwa kituo cha kazi.

Waziri huyo amechukua hatua hiyo kutokana na ujenzi wa barabara ya Njiro-Atomoki iliyopo jijini Arusha yenye urefu wa kilomita 2.8, ambayo imejengwa na kampuni ya Syhydro Constuction Ltd kwa gharama ya Sh bilioni 2.6 kusuasua. Jafo alitoa agizo hilo jana wakati akikagua barabara hiyo ambayo inatakiwa kukabidhiwa serikalini Agosti, mwaka huu.

“Haiwezekani Rais John Magufuli atoe fedha nyingi halafu wananchi hawajui kinachoendelea hapa, ninyi ndiyo mnaohujumu miradi halafu mnasema serikali haijafanya kitu.”

“Sasa ndugu yangu nakwambia kazi yako ya kuwa meneja wa Tarura katika jiji hili imeisha leo na naagiza upelekwe halmashauri nyingine, hapa hapakufai,” alisema.

Awali, Jafo alitembelea Hospitali ya Wilaya ya Arusha nakumtaka mkandarasi anayejenga hospitali hiyo kurekebisha ukuta uliopinda na kuagiza mkandarasi huyo akatwe fedha kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo kwani alishaongezewa muda baada ya muda wake wa awali kwisha.

Mradi huo wa ujenzi wa hospitali ya wilaya umegharimu Sh bilioni 1.4 na hadi sasa mkandarasi ameshalipwa Sh milioni 731.95, ambapo ikamilika itatoa huduma za afya ya uzazi kwa kinamama zaidi ya 200,000 na watoto chini ya miaka mitano zaidi ya 100,000.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi