loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Liverpool yakaribia kuweka rekodi ya pointi Ligi Kuu

MOHAMED Salah, alifunga mara mbili na kusaidia mabingwa Liverpool kufi kisha pointi 92 baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Brighton and Hove Albion kwenye mechi ya Ligi Kuu England juzi.

Ushindi huo unaifanya Liverpool kufikia mapengo yake ya kuweka rekodi kwa kwa kutwaa ubingwa na pointi nyingi, huku kikosi cha Juergen Klopp kikihitaji pointi tisa katika mechi nne zilizosalia kuizidi Manchester City iliyotwaa ubingwa wa msimu wa mwaka 2017/18 kwa kufikisha pointi 100.

Kwa mabao hayo, Salah sasa amefikisha mabao 19, matatu nyuma ya mchezaji wa Leicester City, Jamie Vardy, wanaowania pamoja kiatu cha dhahabu. Akizungumzia suala la pointi, Klopp alisema hana uhakika na utaratibu huo wa kuweka rekodi.

"Si muhimu kwangu, sina uhitaji wowote kwenye hilo, lakini nataka kushinda mechi. Kwa watu wa michezo kwa ujumla inaweza kuwa na umuhimu wake, sisi ni mabingwa na inaweza kuwa vyovyote vile.”

"Kwa sasa tumefikisha pointi 92 na mismu uliopita tulikuwa na 97. Tumepata pointi tano zaidi, siamini, sina hata mawazo imekuwaje tumefika hapa.”

Liverpool itacheza na Burnley iliyo nafasi ya nane kwenye msimamo, mechi hiyo itachezwa kwenye uwanja wa Anfield, ikifuatiwa ugenini dhidi ya Arsenal kabla ya kurudi nyumbani kucheza na Chelsea na kisha kumaliza na Newcastle United kenye uwanja wa St James Park.

WILLIAN ameandika katika mitandao yake ya kijamii kuwa anamaliza miaka ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi