loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mapokezi Simba kufuru

MABINGWA wa tetezi wa Kombe Ligi Kuu Tanzania Bara Simba, wamepokelewa kifalme baada ya kuwasili Dar es Salaamjana wakitokea Ruangwa mkoani Lindi.

Simba walikabidhiwa kombe hilo baada ya kutoka suluhu dhidi ya Namungo FC katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, ambao pia ulitumika kuwakabidhi taji hilo walilolitwaa kwa mara ya tatu mfululizo.

Simba waliwasili Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) saa 2:30 asubuhi, huku umati mkubwa wa wapenzi wa timu hiyo wakijazana kiwanjani hapo kuwapokea.

Nahodha msaidizi wa timu hiyo, Mohammed Hussein ndiye aliyebeba taji hilo walilokabidhiwa juzi Ruangwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla wakiwa na pointi 81 baada ya kucheza mechi 34.

Maelfu ya mashabiki kama ilivyo utamaduni wao walijitokeza kuwalaki wachezaji hao na kuanza kuusindikiza msafara wa kikosi hicho uliokuwa unakwenda Bunju, ambako watapiga kambi kwa ajili ya kuikabili Yanga Jumapili.

Hata hivyo, hatua hiyo ya Simba ya kwenda moja kwa moja kambini, ilikuwa ni kama kuwatelekeza mashabiki wao waliojazana makao makuu ya klabu hiyo barabara ya Msimbazi wakisubiri kuwapokea.

Simba baada ya kutoka JNIA walipita barabara ya Nyerere, Tazara na kushika Mandela, Buguruni, Uhuru na walipofika katika makutano ya Uhuru na Kawawa, walielekea Kawawa na kwenda Magomeni, Morocco na hadi Bunju, ambako wamepiga kambi.

Timu hiyo Jumapili inakutana na watani zao Yanga kwenye Uwanja wa Taifa katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA kuanzia saa 11:00 jioni na mshindi atatinga fainali itakayopigwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.

Mashabiki wa Simba waliokuwa wanasindikiza msafara huo wengine wakiwa na pikipiki na wengine kwa miguu, muda wote walikuwa wakiwashangilia wachezaji wao waliokuwa katika mabasi na magari madogo yaliyokuwa katika msafara mrefu.

Ratiba ya awali iliyotolewa na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ilionesha kuwa baada ya kuwasili kikosi hicho Kiwanja cha Ndege, kikosi hicho kingepita hadi Makao Makuu ya Simba, Msimbazi kukabidhi taji hilo, ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki.

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 3 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 3 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 4 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...