loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba Queens, Yanga vitani leo

LIGI Kuu Soka ya Wanawake inaendelea leo ikiwakutanisha wakina dada wa Simba Queens na Yanga Princess katika mpambano utakaochezwa kwenye Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam.

Ni mchezo wa mzunguko wa 15, ambao kila mmoja anafikiria namna ya kupata pointi tatu na zaidi Simba Queens ikiwa katika presha ya kusaka ubingwa baada ya kuwa katika uongozi kwa muda mrefu.

Wekundu hao wa Msimbazi wanaongoza kwa pointi 35 tofauti ya pointi tatu dhidi ya mabingwa mara mbili mfululizo JKT Queens wanaowanyemelea taratibu wakiwa na pointi 32.

Utofauti huo mdogo wa pointi unawafanya Simba Queens kuwa na presha kwani wasipojitahidi katika mchezo dhidi ya Yanga na wenzao wakashinda mchezo ujao, basi watafikiwa kwa pointi hivyo, kitakachowatofautisha ni magoli ya kufunga na kufungwa.

Pia, Simba Queens inataka kulinda nafasi yake hiyo ya uongozi kwa kuendelea kufanya vizuri ikiwezekana kutwaa taji msimu huu. Yanga inayoshika nafasi ya tano kwa pointi 23 inataka kushinda mchezo huo kulipiza kisasi kwa watani zao ambao tangu walipokutana msimu uliopita wakicheza ligi hiyo kwa mara ya kwanza wamekuwa wakipata vipigo vikali. Waliwahi kufungwa kipigo kizito cha mabao 7-0 kisha mabao 5-1 na mzungumko wa pili msimu huu walifungwa mabao 3-1.

Makocha wa klabu hizo, Mussa Mgosi wa Simba Queens na Edna Lema wa Yanga Princess kila mmoja alisema ni mchezo muhimu kujiongezea pointi tatu na kutimiza malengo waliyojiwekea.

“Sisi tunataka pointi tatu sio tu kwa mchezo wetu dhidi ya Yanga bali michezo yote iliyoko mbele yetu, lengo letu tunataka kuchukua ubingwa msimu huu,”alisema Mgosi. Kwa upande wa Lema alisema “Ni mchezo tunaotaka kufuta uteja na kujenga heshima, tumechoka kufungwa kila wakati ni lazima tupambane kuhakikisha tunashinda,”. Mchezo wa kwanza Simba ilishinda mabao 3-1.

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 3 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 3 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 4 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...