loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanaohamia CCM wasafishiwa njia

MAELEZO aliyotoa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli, yamesafisha njia kwa wapinzani waliojiunga na chama hicho katika siku za hivi karibuni.

Alitoa maelezo hayo mjini Dodoma jana wakati akijibu swali mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Sojo kutoka mkoa wa Songwe kwenye kikao cha NEC.

Sojo alisema kuwa Wanasongwe wanasononeka, pale ambapo wapinzani wanapohamia CCM, wanapewa kipaumbele cha uongozi na kuwaacha wanachama ambao walikipigania chama kufa na kupona 2010-2015.

Sojo alitoa mfano wa majimbo ya Momba na Tunduma. Rais Magufuli alisema kuwa suala hilo, linastahili kuzungumzwa kwenye vikao vya CCM vya wilaya na mikoa, kama wanaokuja wanawahitajika au la.

Alisema kwamba CCM ni chama cha watu, kina misingi yake na kinameza watu wote.

“Suala hilo lizungumziwe kwenye Kamati za wilaya na mikoa na mlitafutie ufumbuzi” aliagiza Mwenyekiti huyo Taifa wa CCM.

Rais Magufuli pia alisema kuwa CCM ina watu wengi ambao walikuwa vyama vingine na aliwataja baadhi ya watu hao kuwa ni Makongoro Nyerere na Stephen Wassira, ambao walikuwa chama cha NCCR Mageuzi, lakini sasa hivi ni “CCM damu damu”.

Aliwataka wanaCCM kuwa na mioyo ya kuvumiliana na kumtanguliza Mungu. Alisema wasiwasi kuwa labda anayefika huenda akawashinda, haupaswi kufikiriwa, kwani upo ukweli kuwa pamoja na kujiandaa, alikuwa anawatandika.

“Tatizo moja la siasa zetu tunajiwekea vizingiti, kwamba akija huyu atashinda, lakini mkiachiwa ninyi hamshindi. Nafikiri meseji mmeipata”alisema Rais Magufuli.

“Lakini Chama hiki kinapokea watu wote ilimradi wanazingatia masharti ya Chama. Sasa mkiingia kwenye ‘group’ zenu za kuanza kubishana mbona amerudishwa huyu! Amerudishwa kwa misingi kwamba mlimzuia njia akapitia dirishani, amerudi sasa apitie mlangoni, mnataka tena mmzuie! Muwe na uvumilivu. Ningependa huyo aliyeingia aendelee kushinda ili siku moja aingie kuwa mjumbe wa NEC,” alisema Magufuli.

Rais Magufuli aliangusha kicheko kwa watu, baada ya kutoa mfano wa mke au mme aliyekuja kuomba msamaha.

"Kwani utakataa? Siyo ajabu akaja na mapenzi mazuri mazuri kuliko ya zamani na amejifunza huko mbinu nyingi na mbadala, Sasa unakataa uhondo huo?” alisema.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi