loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maonesho Sabasaba yamekuwa na tija kwa TRA - Kayombo

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema ushiriki wao katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), umejibu maswali mengi ya msingi ya wananchi wanaotaka kuanzisha biashara na kuziendesha kisheria.

Akizungumza kwenye banda la mamlaka hiyo jana katika viwanja vya sabasaba jijini humo, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo alisema maonesho hayo yamekuwa na tija, kwani baadhi ya huduma kwa wateja zimekuwa zikiendelea kutolewa viwanjani hapo kama kawaida.

Kayombo alisema wananchi wengi wanaotembelea maonesho hayo, wamekuwa wakitembelea banda la TRA kupata elimu ya jinsi ya kuanzisha biashara na kujua jinsi ya kutumia mashine za kodi za kielektroniki (EFDs). Alisema katika banda hilo, wananchi wanahudumiwa, mfano kulipia kodi ya majengo na kodi nyingine sambamba. Pia mtu wanaelezwa jinsi ya kupata mashine ya EFDs.

Pia,Kayombo alisema mwezi huu ni wa kutoa shukrani kwa walipa kodi ambao wamewezesha serikali kuendeleza na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya, elimu na miundombinu mingine.

“Tumefanya Julai kuwa mwezi wa shukrani kwa walipakodi, wamehamasika kwa hiari kulipa kodi na kwa wakati. Kodi hizo zimewezesha mambo mengi ya serikali kutekelezeka. Mishahara inalipwa kwa kodi hizo. Miradi mikubwa ya serikali inaendelea kwa kodi na sekta zote ni fedha za kodi. Tuna kila sababu kuwashukuru walipakodi,”alisema Kayombo.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi