loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wateja wakubwa Tanesco wafungiwa luku mpya

SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco) limeanza mchakato wa kubadilisha mita za umeme kwa wateja wakubwa kutoka mfumo wa zamani wa malipo baada ya matumizi na kuwafungua luku zenye mfumo mpya wa kununua umeme na kisha kuingia moja kwa moja.

Hayo yamebainishwa jana na Ofisa kutoka Idara ya Wateja Wakubwa Upimaji Umeme Tanesco, Matilda Cassian alipokuwa akizungumza na HabariLeo kwenye banda la shirika hilo katika viwanja vya Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba.

Alisema Tanesco iko kwenye mpango wa kubadilisha wateja wakubwa wa umeme wanaotumia T 2 na T 3, ambao hutumia mita na kulipa umeme baada ya kutumia na kwamba mpango huo ukikamilika watakuwa wanatumia luku mpya .

“Tuko kwenye mchakato wa kubadilisha mita za wateja wakubwa wa umeme wa T 2 na T 3 ,wao wanalipwa baada ya kutumia umeme sasa tutawafungia luku za kisasa ambazo ukinunua umeme unaingia moja kwa moja bila mteja kuanza tena kuingiza zile namba za umeme kwenye luku,” alisema Matilda.

Alisema baada ya mfumo huo kukamilika kwa wateja wakubwa wa umeme, utaratibu huo utaendelea kwa wateja wadogo wakiwemo wa majumbani.

“Tukimaliza kwa wateja wakubwa tutaanza kwa wateja wadogo wa T 1 na T 4 ili kuondoa kero ya sasa ambapo mteja akinunua umeme hulazimika tena kwenda kuingiza kwenye luku, tukizibadilisha tuweke zenye mfumo ambao ukinunua tu umeme unaingia moja kwa moja,”alisema Matilda.

Kaimu Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji alisema shirika hilo linaenda na kasi ya mabadiliko ya teknolojia na kwamba inapotokea jambo jipya lenye tija hulichukua na kulifanyia kazi.

“Tumesikia kuna vijana wengi kutoka vyuo mbalimbali vikuu hapa nchini kama Chuo Kikuu cha Dodoma na vingine wamebuni kifaa kinachowekwa kwenye luku kumuwezesha mteja kupitia simu yake kununua na kuingiza umeme bila yeye kuwepo eneo la luku yake ni jambo zuri sana na Sisi yupo tayari kufanya nao kazi,” alisema Leila.

Aliongeza shirika linahitaji teknolojia rahisi na hasa ambazo zinatengenezwa na vijana wa hapa nchini, hivyo kupitia kitengo cha Tehama cha Tanesco wanawakaribisha wale wote wenye bunifu zitakazosaidia kuboresha utoaji wa huduma ya umeme.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi