loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba, Yanga timu bora ishinde uwanjani

MIAMBA ya soka Simba na Yanga kesho zinatarajiwa kumenyana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wa nusu fainali wa michuano ya ASFC, kuwania kutinga fainali.

Kimtazamo ni mchezo mkubwa ambao umevuta hisia za mashabiki na wadau wengi wenye mapenzi na timu hizo pamoja na wapenzi wa mchezo wa soka. Inafahamika pindi timu hizo zinapokutana mambo hujitokeza ikiwemo kejeli za mashabiki wa kila upande kila mmoja akimtambia mwenzake.

Ni jambo zuri hasa ukizingatia timu hizo mbili zinahusishwa na jina la utani, ambalo ukiacha dakika 90, mambo yao mengi hufanya kwa kushirikiana kama ndugu.

Pamoja na porojo zote hizo kitu cha msingi watu wanataka kuona burudani kwenye mchezo huo na sio vita na mapambano, ambayo yataleta majuto baada ya filimbi ya mwisho.

Mara nyingi timu hizo zinapokutana ile kauli ya utani huwekwa pembeni na kugeuka vita jambo ambalo lilisababisha viti kuvunjwa na mashabiki na wachezaji kupigana.

Ninavyo fahamu vita mechi ya Simba na Yanga ni vita ya dakika 90 ndani ya uwanja baada ya hapo wachezaji wa pande zote mbili huwa marafiki kupeana mikono na jambo linakwisha.

Ni kweli mchezo wa kesho unapresha kubwa sana kwasababu wanawania kucheza fainali lakini kwa ukomavu na uzoefu wa timu zote mbili haitarajiwi kuona mpira wa vurugu na mapambano yasiyokuwa na maana.

Itapendeza kuona kila upande ukichanga karata zake vizuri na kuonyesha mbinu zao ili kupata ushindi ambao utathibitisha ubora wao na kwa mashabiki wao.

Simba inatajwa ndio timu bora kwa msimu huu kwa timu za Ligi Kuu, takwimu hizo zinatokana na mafanikio waliyoyapata kwa kutwaa ubingwa wa ligi kwa misimu mitatu mfululizo lakini hata uwezo wa mchezaji mmoja mmoja.

Lakini kwenye mechi ya watani hicho hakiangaliwi sana kwani ukiangalia hata kwenye ligi timu hizo zilipokutana kwenye mechi mbili Yanga ameambulia pointi nne kati ya sita na Simba amepata pointi moja mbele ya timu inayotajwa kuwa na kikosi dhaifu.

Waamuzi nao wanapaswa kuwa makini na kusimamia sheria 17 ipasavyo ili kuondoa lawama na hisia za uonevu kwa kila upande na mshindi apatikane kihalali, baadhi ya mechi za Simba na Yanga huko nyuma ziligubikwa na malumbano kutokana na mwamuzi kushindwa kulimudu pambano.

TFF pamoja na Bodi ya Ligi wanapaswa kuwa makini katika kumteua mwamuzi wa mchezo huo ili kuhakikisha mshindi anapatikana kihalali na wachezaji wa pande zote baada ya dakika 90 wanapeana mikono.

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 4 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Kila mchezaji wa kigeni mil 4

masaa 4 yaliyopita Rahel Pallangyo

KLABU ya ...

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

masaa 5 yaliyopita Mohammed Mdose

SIKU moja ...